Mfanye Mungu Ageuze Hukumu Yake Kwako

Mfanye Mungu Ageuze Hukumu Yake Kwako

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,119
Reaction score
1,570
Yer 18:8 SUV
[8] ikiwa taifa lile nililolitaja litageuka, na kuacha maovu yake nitaghairi, nisitende mabaya yale niliyoazimia kuwatenda.

Kupitia kinywa cha nabii Yeremia, Mungu anazungumza kuhusu mamlaka aliyonayo kama mfinyanzi wa mataifa, anaeleza wazi ile hukumu aliyotoa kwao kulikuwa na nafasi ya kubadilika.

Nini kinafanya hukumu ya Mungu ibadilike juu ya mtu huyo? Unaweza kujiuliza hilo, jibu lake lipo wazi, ikiwa mtu au watu wataacha njia zao mbaya Mungu alikuwa na uwezo wa kughairi mabaya juu ya hao watu..

Tunapotazama jambo hili katika agano jipya, tunaona Yesu alisisitiza sana kuhusu toba, hii ilikuwa ni msingi wa kuingia katika Ufalme wake.

Mt 4:17 SUV
[17] Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

Mungu hapendezwi kabisa na matendo yetu mabaya, na ameweka wazi hukumu ya watenda mabaya, ila ana huruma. Sio hivyo tu, Mungu anataka kuona mabadiliko ya moyo wa mtu mbaya.

Mtu yeyote yule, hata kama alikuwa mchafu sana, hata kama alikuwa ni tishio baya katika Dunia hii kwa matendo yake maovu. Akienda mbele za Mungu kufanya toba ya kweli, mtu huyo atapata msamaha na uzima wa milele itakuwa ni halali yake.

Lk 15:7 SUV
[7] Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.

Mtu aliyeonekana hafai kabisa, anaweza kufanywa upya akafaa, pale tu atakapoamua kuacha njia zake mbaya na kumkimbilia Bwana Yesu.

Tuliona neno la msingi hapo lilionyesha Mungu anaweza kughairi mabaya kwa watu wake, pale watu watakapobadilika kwa kutubu na kuziacha njia zao mbaya. Ndivyo anaweza kughairi na kwako, hapa ni kwa wale tu wanaotubu na kuanza upya na Mungu.

Tunaweza kutumia fursa hii ya upendo wa Mungu kwetu, kurejesha mahusiano yetu upya na Yeye, tutaona utamu wa kuokoka ulivyo mzuri.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom