Mfahamu mchezaji msomi wa Coastal Union

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,258
Kutana na Daktari Mtarajiwa Anayekipiga Coastal Union

Si aghalabu sana kukuta wanasoka wa Tanzania wenye taaluma zao lakini pia wapo wanaosema mshika mbili, moja humponyoka, lakini mbele ya kijana Ayoub Idrisa Semtawa ni tofauti, kwani ameweza kumudu masomo yake vizuri pamoja na soka pia.
Akiwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), tayari Ayoub ni mchezaji wa klabu ya Ligi Kuu ya Bara, Coastal Union ya Tanga wa pili kutoka kushoto waliosimama




 
Kumbe mwaka wa pili chuo ndio 'msomi'? Hakuna wachezaji wengine wanaosoma chuo au?
 
Dokta anashuka daraja,ingebidi na dokta ahamishiwe tandabui akapige diploma in clinical medicine.
 
Nilijua ameshamaliza Na ni daktari kamili kumbe bado mwanafunzi...!!! Kila la Heri kwake.
wale watangazaji aidha walikua wanapotosha au hawajui mfumo wa taaluma hii lakini huenda tatizo linakuzwa mahala pengine na kuambukiza kwa hiyo nimeliweka kibega
 
Very interesting, anamudu medicine na kuchezea coastal union.
Medicine kwani ni kitu gani mzee? Stephen Hawkings unamjua? Ubongo wake umepata tatizo 99% na anatumia 99% ya 1% ilobakia lkn ndio mwana sayansi prof wa hesabu pekee & cosmology na amekalia dawati ya Isaack Newton pale Havard.

Ubongo una nafasi kubwa mno ya kujua mambo, usidhani medicine ndio yardstick ya kitu kigumu
 
Dogo aliacha shule mwaka 2013 ... Sasa, sijui kama alirudi tena. Ngoja niulizie kwa classmates wake nitarudi.

Kuhusu kujua mpira, hilo halina shaka..!
 
sentenso imeanza na si aghalabu.............................................ndio maana hata wewe umemkumbuka mmoja tu wa MIAKA HIYOOOOOOOOOOOOOO
Mbona hata tenga kachezea pan African akiwa msomi mwenye degree?
 
Back
Top Bottom