barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Sakata la Makonda lachukua sura mpya, Mameya na Madiwani kutoshirikiana na RC
Diwani wa kata ya Ubungo na mstahiki Meya wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo na katibu wa madiwani wa CHADEMA Tanzania,Boniface Jacob ni mwalimu kitaaluma toka UDSM.
Boniface amekuwa akiandika mambo kadhaa katika mitandao ya kijamii,akiwa na lengo la kutoa ufafanuzi wa kitu fulani.Ameandika mengi kuhusu Bashite na sasa ameandika waraka mrefu kuhusu kukataa Jiji la Dsm kuwa chini ya "kilaza".
Sina tatizo na hoja za Meya Boniface,wala maandishi anayokuwa anaandika,hoja yangu kubwa ni namna ya uandishi.Nyingi ya mabandiko ya Meya Boniface hayafanyiwi uhariri.
Kwa kiongozi aina ya Boniface,maandishi yake yanapaswa kuwa yamehaririwa kabla ya kuifikia hadhira,hii ni kutokana na heshima na cheo alichonacho mbele ya jamii.
Mara nyingi sana katika maandishi yake amekuwa akichanganya sana,sehemu ya herufi kubwa anaweka ndogo na sehemu ya herufi ndogo inakaa kubwa.Alama kama nukta,mkato,alama ya kuuliza,alama ya kushangaa nk hazipewi nafasi.Wapo "member" wengi humu JF wamekuwa wakikosoa sana aina hii ya uandishi ya huyu kiongozi.
Ukiangalia ktk maandishi aliyoandika kukataa ushirikiano na "Bashite" wa Dsm kuna maneno mengi yasiyohaririwa,hayo ni kama "kashfa ya kugushi vyeki",haharani,ajawahi,narabara n.k
Maandishi yake yanasomwa na watu wengi,vijana wengi wanatakiwa kujifunza kwa viongozi wa aina ya Meya wa Ubungo.Boniface kwa sasa ni "role model" wa vijana na hata watu wazima,itapendeza kama maandishi yake yatafanyiwa uhariri wa kutosha kabla ya kutoka hadharani.
Meya Boniface anatakiwa kujua,kwa nafasi yake kama meya,maandishi yake yatatumika kama nukuu na watu mbalimbali,nukuu ktk mikutano ya kisiasa au maandishi ya uchambuzi wa mambo ya kisiasa.Anatakiwa kuwa makini ili kuwafanya wale wote wanaopenda aina ya mijadala na maandishi yake kutopata shida ya kuchomoa sehemu ya maandishi yake kama rejea na nukuu.
Viongozi na watu wote maarufu duniani huacha rejea na nukuu kutoka ktk matamshi yao,hotuba zao na maandishi yao.Kama hotuba,maandishi na matamshi yao yatakuwa katika lugha isiyohaririwa,italeta mtafaruku mbele ya safari.
Nukuu za hotuba na maandishi ya Mwalimu Nyerere,zipo hivyo mpaka leo,sababu ziliandikwa na kutamkwa katika lugha sahihi.Nukuu za watu wengine maarufu kama Mandela,Mugabe,Jakaya Kikwete,Mwinyi na Mkapa,zipo hapo zilipo sababu ya usahihi wa namna zilivyoandikwa na kutamkwa.
Maandishi,hotuba na matamshi huishi,huendelea kumtambulisha mtu/kiongozi hata baada ya kufa.Kuna misemo na hotuba za "mzaha" na "futuhi" zilizoandikwa na kutamkwa lkn bado zinaendelea kuwa rejea na nukuu sababu ziliandikwa kwa "uhariri" kwa kiwango bora kwa hadhira.
Hii ni kwa Mstahiki Meya wa Ubungo,sababu si mara moja au mbili,mabandiko yake katika ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Facebook,yamekosa "uhariri" wa kiwango cha diwani na meya wa Ubungo.
Ushauri huu ni kwa nia njema,ndio maana watu kama Zitto Kabwe,maandishi yake katika ukurasa wake wa Facebook na Twitter hunakiliwa na magazeti yenye hadhi Tanzania kama makala,sababu lugha inayotumika na uhariri wa habari kabla ya kuifikia hadhira,huwa ni wa kiwango bora zaidi.
Hii ni maalumu kwa Mwalimu Boniface Jacob a.k.a Jonas Savimbi.Mlinzi wa zamani wa Freeman Mbowe na "Senior Councilor" wa Ubungo
Meya Boniphace Jacob amfungukia RC Makonda
Salam za Mstahiki Meya Boniface Jacob kwa Mh Aikael Mbowe
Ukipitia "thread" hizo hapo juu,ambazo ni "copy and paste" kutoka kwenye ukurasa rasmi wa Fb wa Boniface Jacob,utabaini hiki kinachoongelewa.