Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Habari wanaJF,
Isaya Charles Mwita ambaye ni mstahiki Meya ya Jiji la Dar es Salaam ameeleza historia ya maisha yake alipokuwa akihojiwa na muandishi wa gazeti la Raia Mwema. Mstahiki meya wakati wa mahojiano alibainisha kwamba yeye ni muhitimu wa fani ya Uchumi kutoka chuo cha Mwalimu Nyerere Memorial Academy kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Ingawa mheshimiwa hakusema ni alihitimu astashahada, stashahada, shahada, uzamili wala uzamivu.
Pia katika kuiendeleza fani yake ya uchumi na kubobea zaidi mstahiki meya anasema alibahatika kuisaidia Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa utaratibu wa kujitolea kama mchumi.
Aidha mstahiki meya alielezea historia yake kwa ufupi kuwa amepitia maisha yenye changamoto nyingi sana kwani mwaka 1976 baba yao mzazi aliwaacha wakiwa wadogo, pia hakufaulu mtihni wa kumaliza elimu ya msingi hivyo ilimbidi arudie darasa tena yaani (kukariri) ndipo akapata nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari.
Nadhani kwa waliokuwa hawafahamu kiwango cha elimu ya meya watakuwa wamepata mwanga.
Ahsante