Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amewataka wakazi wa jiji hilo ambao hawajayaendeleza maeneo yao na kusababisha vichaka karibu na makazi ya watu kuyaendeleza, kinyume na hivyo maeneo yao yatachukuliwa na serikali.
Akizungumza na gazeti hili, Mwita alisema yapo malalamiko kutoka kwa wananchi wa maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam kuzungukwa na vichaka na magofu ya nyumba ambayo yamekuwa maficho ya wahalifu na hivyo kuhofia usalama wao.
“Nawapa pole wananchi wote ambao wamepatwa na maswahibu mbalimbali ya mali zao kutokana na hali hiyo, lakini niwahakikishie kwamba jiji lina mipango kabambe ya kuendeleza jiji kulifaya kuwa la kisasa,” alisema.
Alisema; “Julai 18 mwaka huu tutarusha ndege kwa ajili ya kumalizia mpango kazi wa Jiji la Dar es Salaam na tukimaliza Septemba tutakuwa na kitu cha kufanya na ni mapema kukisema kwa sasa. Tunataka Dar es Salaam iwe na heshima kama miji mingine ingawa tunajua itachukua muda”.
Alisema kuendeleza au kutoendeleza ardhi kunategemeana na sheria jinsi ilivyo na hata Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendelea kufuta hati za watu kutegemeana na hali ilivyo.
Ofisa Habari wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera alisema Manispaa hiyo imekuwa na utaratibu wa kusafisha maeneo yenye vichaka mara kwa mara kudhibiti uhalifu.
“Kama mtu ana eneo lake ambalo lina kichaka na hasafishi ni kosa na ni kinyume cha sheria. Hata kama halijapimwa ni lazima liwe safi. Tunatumia Kata na Mitaa kukagua maeneo husika.Kama kuna watu bado wana mapori wasafishe” alisema.
Naye mkazi wa Chanika, Juma Abdul, alisema kuwepo kwa vichaka katika maeneo yao kumesababisha uhalifu wa mara kwa mara.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyakwale, Kibada ambako kuna maeneo mengi hayajaendelezwa, Said Pazi alisema vichaka hivyo vimekuwa tatizo kwao na kuchangia uhalifu wa mara kwa mara na wakati mwingine mauaji.