Meya wa Ilala Charles Kuyeko, Atimiza Ahadi Yake kwa Wananchi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala mhe. Charles Kuyeko ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bonyokwa kupitia Chadema ametimiza ahadi yake aliyoitoa kwa wananchi wa Kata ya Bonyokwa katika kampeni za kuomba kura ya udiwani.

Moja ya ahadi alizoahidi mhe. Kuyeko ni kuhakikisha kuwa Bonyokwa inakuwa na miundombinu ya barabara imara zinazopitika wakati wote.

Katika kutekeleza ahadi hiyo mhe. Kuyeko Leo amesimamia makabiziano ya daraja la chuma litakalokuwa kiunganishi cha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi. Daraja hilo limejengwa maeneo ya mtaa wa Kisiwani. Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutawaondolea adha ya usafiri wananchi wa Kata hiyo. Daraja hilo ni kiunganishi muhimu sana kwa wananchi wa Kata ya Kinyerezi na Kata ya Bonyokwa ambapo kabla mawasiliano ya barabara yalikuwa yalikuwa ya mashaka hasa wakati wa mvua.

Mhe. Kuyeko anatimiza ahadi hiyo ya kuwajengea daraja wananchi wa Kata ya Bonyokwa ikiwa ni takribani miezi Sita toka achaguliwe kuwa Diwani wa Bonyokwa na ni miezi takribani minne toka achaguliwe kuwa Meya wa Manispaa ya Ilala.

Wakizungumza katika hafla hiyo wananchi wa Kata hiyo wamempongeza mhe. Kuyeko kwa kuwatatulia kero hiyo ya daraja, tena kwa muda mfupi sana. Wananchi wanasema CCM wameongoza eneo hili toka Tanzania ipate Uhuru lakini walishindwa kutusaidia kupata daraja iweje Leo Kuyeko ajenge daraja ndani ya miezi sita tu?

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kisiwani CCM, ndugu Peter amemshukru mhe. Kuyeko kwa juhudi zake za kuhakikisha anaimarisha miundombinu ya barabara, peter ameahidi kushirikiana na wananchi wa eneo hilo kuwa watalilinda daraja ili litumike kwa muda mrefu.

Mhe. Kuyeko amewahakikishia wananchi wa Bonyokwa kuwa atatimiza ahadi zake zote. Pia amesema barabara ya Segerea kwenda Bonyokwa itaanza kujenga hivi karibuni Mara baada ya mvua kukatika kwani tayari mkataba umesainiwa na barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami.

Kuyeko pia amezungumzia kuimarisha barabara ya Kinyerezi kwenda Msingwa, kituo cha daladala na soko katika mtaa wa Msingwa, ambapo alisema mipango inafanywa ili kuanza ujenzi Mara moja. Mhe. Kuyeko amesema dhamira yangu ni kuhakikisha mitaa yote ya Kata ya Bonyokwa inaunganika na kuwa na muingiliano wa watu wake wakati wote tofauti na ilivyo sasa.

Mhe. Kuyeko amewaomba wananchi wamuunge mkono katika kupigania maendeleo ya wanabonyokwa, kwani maendeleo hayana itikadi.

Aidha, Makabidhiano hayo ya daraja hilo yamefanyika baina ya mhandisi wa Manispaa ya Ilala na mhandisi wa TANROADS wa Wilaya ya Ilala. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia maafisa mbalimbali wa Ilala, Diwani wa Liwiti mhe. Edwin Mwaipaja na mhe. Greyson Celestine Diwani wa Kinyerezi.

Imetolewa Leo 29/04/2016
Na Alex Massaba
Katibu wa Meya Manispaa ya Ilala
0656 568256
IMG-20160429-WA0063.jpg
IMG-20160429-WA0068.jpg
IMG-20160429-WA0064.jpg
IMG-20160429-WA0067.jpg
 
alafu watu fulani wanataka wawakwamishe UKAWA katika kuleta mabadiliko Dar es Salaam, kwa maana nyingine tuendelee na uduni na ujinga waliotutengenezea.
 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala mhe. Charles Kuyeko ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bonyokwa kupitia Chadema ametimiza ahadi yake aliyoitoa kwa wananchi wa Kata ya Bonyokwa katika kampeni za kuomba kura ya udiwani.

Kwa mara ya kwanza toka CHADEMA ianzishwe leo ndio nakutana na kiongozi wa CHADEMA aliyetimiza ahadi aliyotoa kwa wananchi.

HONGERA mheshimiwa mstahiki meya Kuyeko
 
Kweli kuchanganyikiwa nikubaya wafanya maiguzo niwakinanani?
 
View attachment 343524 View attachment 343525 View attachment 343526View attachment 343528
Hii habari ni mbaya sana kwa ustawi wa ccm jijini dsm
 
alafu watu fulani wanataka wawakwamishe UKAWA katika kuleta mabadiliko Dar es Salaam, kwa maana nyingine tuendelee na uduni na ujinga waliotutengenezea.
Baada ya miaka 54 ya uhuru!!!!!
 
Kwa mara ya kwanza toka CHADEMA ianzishwe leo ndio nakutana na kiongozi wa CHADEMA aliyetimiza ahadi aliyotoa kwa wananchi.

HONGERA mheshimiwa mstahiki meya Kuyeko
Tunashukuru kwamba mmeanza kuisoma namba,pongezi pekee zimwendee marehemu john komba kwa wimbo wake
 
Back
Top Bottom