Meya wa Dar kupitia upya mikataba ya UDA, DART na stand ya Ubungo

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Charles Mwita, amesema mikataba tata iliyoingiwa na Jiji ukiwamo ule wa mabasi yaendayo kasi (Dart) na Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) pamoja na ule wa Kituo cha Mabasi Ubungo, itapitiwa upya na wanasheria kisha taarifa zake kuwekwa wazi kwa umma.

Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum mwishoni mwa wiki, Meya Mwita alisema: “Tutaita wanasheria na tutaipitia hadharani na tutawaeleza wananchi. Nina siku tatu ofisini, nipeni muda zaidi nitaeleza tuliyobaini kwenye mikataba husika.”

Meya huyo ambaye alichaguliwa na madiwani wa Chadema na wa CUF, alisema hakutakuwa na ubabaishaji katika mikataba hiyo kwani ndiko mapato mengi yanakopotea na kusababisha miradi ya maendeleo inayohudumia wananchi wengi kukwama ama kutotelekezwa.

“Ninachotaka bora mimi nife, lakini wananchi mpate haki, mmekuwa maskini kwa muda mrefu sana, mmedharauliwa vya kutosha, haiwezekani nchi ni yetu sote, siyo ‘majitu’ fulani yanakuja hapa yanatengeneza genge la wizi na kutajirika, wakati raslimali zipo na fedha za kutekeleza miradi ipo, kinachotakiwa ni usimamiaji na ufuatiliaji kuhakikisha hakuna shilingi inapotea,” alisisitiza na kuongeza.

“Tutaheshimiana hapa mjini, Mungu ndiye ametupa Dar es Salaam, tutawatumikia sana kwa nguvu zote,” alisema Mwita ambaye ni diwani wa kata ya Vijibweni.

Meya huyo alianza na mradi wa Uda kuwa atahitaji ripoti kutoka kwa waliokuwepo na kusoma kwa undani ndipo atakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia.

"Kituo cha Ubungo, mwaka jana kulikuwa na mpango wa kukihamisha kwenda Mbezi, lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika, ninachosubiri ni ripoti ya kwanini waliamua kubomoa kabla hawajamaliza kujenga kituo mbadala," alisema na kuongeza.

“Tutaamua kwa pamoja katika kikao chetu cha Jiji kwamba tutaendelea na kituo kilichopo au Mbezi. Nina jambo la dharura nitakwenda kulifanya juu ya kituo hiki ambacho kinatoza fedha kwa watumiaji, lakini hakuna huduma za choo, kujikinga na jua na mpangiliop kwa ujumla,” alisema.

BODABODA
Meya huyo alisema hatakubaliana na kamatakamata ya waendesha pikipiki inayofanyika maeneo mbalimbali ya Jiji kwa kuwa vijana wanajitafutia riziki ya kuendesha familia zao.

“Hawa ni Watanzania wenzetu ambao serikali iliwanyima elimu, mtu akijiajiri tumuonee huruma, tumsaidie na siyo kumfanya awe maskini zaidi,” alisema.

Meya Mwita alisema suala la pikipiki kuingia katikati ya Jiji litajadiliwa kwenye vikao na kusikiliza walioamua kuwazua kwanini walifanya hivyo na kama inawezekana kuweka utaratibu wa muda wa kuingia na kutoka.

Alisema wengi wanakamatwa kwa makosa ya leseni, lakini kinachoonekana ni kukosekana kwa elimu, hivyo Polisi na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuwaelimisha umuhimu wa kuwa na leseni na bima za vyombo vyao.

“Nitaendelea kutoa elimu kwenye vyombo vya habari, nitawakusanya waendesha bodaboda wote nitaongea nao, pia madiwani wa vyama vyote tujadili kwa kina na kuwa na utaratibu maalum kwa ajili yao nao watoe elimu ya uraia kwenye kata zao,” alisema.

Chanzo: Nipashe
 
Hayo yote yatahamishiwa mamlaka nyingine
Nchi hii ni kituko, baada ya kuona majiji makubwa mengi yameshikwa na upinzani nasikia Serikali imeanza kubadirisha baadhi ya Sheria/Taratibu za makusanyo ya Property Tax, kwasasa makusanyo haya yatakua chini ya TRA badala ya Halmashauri ili upinzani usije ukiwafunika katika makusanyo katika Halmashauri, Sitaki kuamini kwamba hata Magu ameishaingia kwenye huu mtego wa uchama chama
 
Viva ukawa, nadhani uhuni jijini daa sasa unaanza kupata muarobaini..
Huu mwanzo mzuri sana mkuu.
MKipindi kile Mwanza imekamatwa na CDM walifanya figisu sana mpaka zikazuiliwa Billioni zaidi ya 40 kwenda jijini ambazo zilikua ruzuku ya jiji.

Sasa mwaka huu usishangae kusikia zimezuiliwa nyingine
 
Kweli mkuu watafanya makusud ili ionekane ukawa hawana jipya but naamini kwa mikataba mingi mibovu iliyoingiwa ukweli tutaupata very soon!
 
Na hii mikataba ndio inayomfanya Makonda aweweseke kuwafichia maovu yao mabwana zake waliomuweka mjini, ile kelele ya kuwa yeye ndie rais wa Dar ni sawa na mbwa muoga kumbwekea mpita njia ili bosi aone mbwa wake ni mkali, safari hii watanyooka tu mambo hadharani mchana kweupe.
 
Huu mwanzo mzuri sana mkuu.
MKipindi kile Mwanza imekamatwa na CDM walifanya figisu sana mpaka zikazuiliwa Billioni zaidi ya 40 kwenda jijini ambazo zilikua ruzuku ya jiji.

Sasa mwaka huu usishangae kusikia zimezuiliwa nyingine
Kweli mkuu watafanya figisu jiji likose fedha iliionekane ukawa hawana ishu but ni mwanzo mzuri wakujua mikataba mibovu iliyoingiwa na ninani waliosababisha..
 
Huyu Meya nafikiri siyo UKAWA! Matendo yake na dhamira yake ya kuwakomboa wana Dar zinafanana na za Rais wetu Magufuli! Aidha Magufuli anatekeleza Ilani ya UKAWA (kama wanavyodai) au huyu Meya anafuata nyayo za Magufuli za "Hapakazitu"!
 
Nchi hii ni kituko, baada ya kuona majiji makubwa mengi yameshikwa na upinzani nasikia Serikali imeanza kubadirisha baadhi ya Sheria/Taratibu za makusanyo ya Property Tax, kwasasa makusanyo haya yatakua chini ya TRA badala ya Halmashauri ili upinzani usije ukiwafunika katika makusanyo katika Halmashauri, Sitaki kuamini kwamba hata Magu ameishaingia kwenye huu mtego wa uchama chama
Miongoni mwa mambo mnakosea watanganyika wengi niile kumtenga Magu...na CCM....!!! kitu ambayo haiwezekani
 
huyo meya hajasoma pubic management na wala hajui kwa nini wabunge wanaapa kulindaa siri za bunge wakati huo huo mijadala ya bunge inaonekana live azam tv. hajui ni kwa nini viongozi wote baada tu ya kiapo cha uaminifu wanaapa kutunza siri ... siri gani hizo ? sasa kama mikataba ya kibiashara huwa ni siri na hulindwa kwa maslahi ya pande zote mbili zinazonufaika na hiyo mikataba.kimsingi matatizo ya wana wa dar es salaam sio kujua siri iliyofichwa kwa miaka mingi ... hapana. jukumu la meya ni moja tu kutatua kero sio kutujaza taarifa sisi wapiga kura ili tufurahi au tusikitike ... achukue hatua. matunda na machungu ya hatua alizochukua ndizo tunazotaka kuziishi
 
wewe boya kweli usiri ndio uliotufikisha hapa, tenda zote zimeitwa kwa uwazi, iweje makubaliano yawe siri?
 
huyo meya hajasoma pubic management na wala hajui kwa nini wabunge wanaapa kulindaa siri za bunge wakati huo huo mijadala ya bunge inaonekana live azam tv. hajui ni kwa nini viongozi wote baada tu ya kiapo cha uaminifu wanaapa kutunza siri ... siri gani hizo ? sasa kama mikataba ya kibiashara huwa ni siri na hulindwa kwa maslahi ya pande zote mbili zinazonufaika na hiyo mikataba.kimsingi matatizo ya wana wa dar es salaam sio kujua siri iliyofichwa kwa miaka mingi ... hapana. jukumu la meya ni moja tu kutatua kero sio kutujaza taarifa sisi wapiga kura ili tufurahi au tusikitike ... achukue hatua. matunda na machungu ya hatua alizochukua ndizo tunazotaka kuziishi

Wewe ndiye umesomea hiyo na wapi ?
Na what the hell is pubic management ??
 
Uovu hauwezi kutunzwa kama siri. Principles of public management tangu lini zikatukuza maovu kuwa siri.

Kumbuka JF ni Gts
 
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Charles Mwita, amesema mikataba tata iliyoingiwa na Jiji ukiwamo ule wa mabasi yaendayo kasi (Dart) na Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) pamoja na ule wa Kituo cha Mabasi Ubungo, itapitiwa upya na wanasheria kisha taarifa zake kuwekwa wazi kwa umma.

Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum mwishoni mwa wiki, Meya Mwita alisema: “Tutaita wanasheria na tutaipitia hadharani na tutawaeleza wananchi. Nina siku tatu ofisini, nipeni muda zaidi nitaeleza tuliyobaini kwenye mikataba husika.”

Meya huyo ambaye alichaguliwa na madiwani wa Chadema na wa CUF, alisema hakutakuwa na ubabaishaji katika mikataba hiyo kwani ndiko mapato mengi yanakopotea na kusababisha miradi ya maendeleo inayohudumia wananchi wengi kukwama ama kutotelekezwa.

“Ninachotaka bora mimi nife, lakini wananchi mpate haki, mmekuwa maskini kwa muda mrefu sana, mmedharauliwa vya kutosha, haiwezekani nchi ni yetu sote, siyo ‘majitu’ fulani yanakuja hapa yanatengeneza genge la wizi na kutajirika, wakati raslimali zipo na fedha za kutekeleza miradi ipo, kinachotakiwa ni usimamiaji na ufuatiliaji kuhakikisha hakuna shilingi inapotea,” alisisitiza na kuongeza.

“Tutaheshimiana hapa mjini, Mungu ndiye ametupa Dar es Salaam, tutawatumikia sana kwa nguvu zote,” alisema Mwita ambaye ni diwani wa kata ya Vijibweni.

Meya huyo alianza na mradi wa Uda kuwa atahitaji ripoti kutoka kwa waliokuwepo na kusoma kwa undani ndipo atakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia.

"Kituo cha Ubungo, mwaka jana kulikuwa na mpango wa kukihamisha kwenda Mbezi, lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika, ninachosubiri ni ripoti ya kwanini waliamua kubomoa kabla hawajamaliza kujenga kituo mbadala," alisema na kuongeza.

“Tutaamua kwa pamoja katika kikao chetu cha Jiji kwamba tutaendelea na kituo kilichopo au Mbezi. Nina jambo la dharura nitakwenda kulifanya juu ya kituo hiki ambacho kinatoza fedha kwa watumiaji, lakini hakuna huduma za choo, kujikinga na jua na mpangiliop kwa ujumla,” alisema.

BODABODA
Meya huyo alisema hatakubaliana na kamatakamata ya waendesha pikipiki inayofanyika maeneo mbalimbali ya Jiji kwa kuwa vijana wanajitafutia riziki ya kuendesha familia zao.

“Hawa ni Watanzania wenzetu ambao serikali iliwanyima elimu, mtu akijiajiri tumuonee huruma, tumsaidie na siyo kumfanya awe maskini zaidi,” alisema.

Meya Mwita alisema suala la pikipiki kuingia katikati ya Jiji litajadiliwa kwenye vikao na kusikiliza walioamua kuwazua kwanini walifanya hivyo na kama inawezekana kuweka utaratibu wa muda wa kuingia na kutoka.

Alisema wengi wanakamatwa kwa makosa ya leseni, lakini kinachoonekana ni kukosekana kwa elimu, hivyo Polisi na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuwaelimisha umuhimu wa kuwa na leseni na bima za vyombo vyao.

“Nitaendelea kutoa elimu kwenye vyombo vya habari, nitawakusanya waendesha bodaboda wote nitaongea nao, pia madiwani wa vyama vyote tujadili kwa kina na kuwa na utaratibu maalum kwa ajili yao nao watoe elimu ya uraia kwenye kata zao,” alisema.

Chanzo: Nipashe
Mungu ibariki UKAWA .
 
Lion Chawene alisema UKAWA tekelezeni sera za Ccm za kulindana na kudai rushwa maana chama chao ndicho kiko madarakani. Angalia wasije kukukolimba.
ccm haiwezi tena kuaminika nchi hii , sakata la rushwa ya wabunge 18 ni kielelezo halisi .
 
Back
Top Bottom