Meya ISAYA MWITA mengine yapitie sikio la kulia yatokee kushoto.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Suala la kuambiwa kua eti chama chako kikikufukuza uende kwa Makuu wa kaya utapewa kazi ni kauli ambazo ni za kisiasa ambazo unaweza kupokelea sikio la kulia zikatokea sikio la kushoto. Hii kauli inaweza kukufanya hata baadhi ya viongozi wako wa chama kushindwa kuielewa kukusababishia misuguano.Lakini kwakua wewe ni mtu makini na mwelewa utakua unajua ni kwanini unasifiwa.Mtendaji bora sio lazima atoke CCM, hata UKAWA/CHADEMA wapo.

Wanatakiwa wafahamu kua ndani ya chadema kuna viongozi imara na makini na mfano wake ni wewe, huwezi kufukuzwa ndani ya chama kwa sababu tu mtu wa CCM amekusifia, inatakiwa ukaze kamba hivyo hivyo ili hata wananchi wakusifu na waone tofauti ya mameya wa CCM na Chadema.

Kumbuka kua CCM hawa hawa walifanya figisu figisu ili ushindwe kuipata nafasi hiyo, lakini kuna makamanda hawakukata tamaa, waliitwa wachochezi wengine walitiwa ndani kwa sababu tu kuna watu hawakutaka Meya wa jiji la DSM na manispaa zake atoke UKAWA.Watumikie wananchi kwa moyo mmoja hao upande wa pili acha waendelee kukusifia.

Wewe ni diwani unayetokana na kura za wafuasi wa vyama vinavyounda UKAWA, walikupa nafsi hiyo uwatumikie wao na wananchi wengine we fanya kazi! Utendaji wako uliotukuka ndio utakaojieleza na naamini hizi sifa unachukulia kama mojawapo ya kukubalika kwako na jamii. Wewe ni MwanaUKAWA mambo ya kazi nyingine tuliambiwa wanapewa makada wa CCM, hivyo hiyo kauli ya kupewa kazi ilikua ni kama kutaka kuwachokoza viongozi wa chama waliokuamini wakapendekeza jina lako kugombea nafasi hiyo.
 
Usiwe na wasiwasi ndugu yangu Rais ameona UKAWA inavyofanya kazi na kusimamia pesa za halmashauri.Amependezwa nalo ila si rahisi kulitoa fully wenye chama chao watamshangaa.
 
Back
Top Bottom