Meya wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mkoani Mwanza Henry Matata amesema kuwa uamuzi wa kuwafukuza madiwani watatu wa CHADEMA katika manipaa hiyo, upo pale pale.
Madiwani hao wamekumbwa na sokomoko hilo, kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila idhini ya mwenyekiti ambaye ni meya.
Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu akiwa mjini Dodoma, Matata alisema uamuzi wa kuwafukuza upo pale pale na kwamba hakuna mamlaka nyingine inayoweza kutengua.
Meya huyo alisema kuwa kinachosubiriwa kwa sasa ni kutangazwa kwa tarehe ya kufanyika uchaguzi mdogo katika kata tatu ambazo madiwani wake walifukuzwa kwa mujibu wa sheria.
Meya huyo ambae alifukuzwa CHADEMA kisha kufungua kesi mahakamani kupinga uamuzi wa Kamati Kuu (CC) alisema yeye hababaishwi na maneno.