Ujio wa kocha Patrick Phiri ulileta faraja kubwa miongoni mwa mashabiki wa timu ya soka ya Simba SC a.k.a Mikia FC au Dar United iliyomaliza katika nafasi ya Nne msimu uliopita.
Aidha usajili wa Emmanuel Okwi uliongeza faraja hiyo huku mashabiki wakiamini kuwa Okwi ni yule yule wa enzi za 5-0 na hata Okwi mwenyewe kipindi akipokelewa na viongozi wa Simba alionesha vidole vyake vitano labda alikuwa anamaanisha kipigo cha 5-0 kwa Yanga kitajirudia kipindi akiichezea Simba.
Katika hali isiyotegemewa Simba imeanza vibaya kwa kutoa sare kila mchezo iliocheza isipokuwa mchezo kati yake na Yanga ambapo ilitoa suluhu. Kwa matokeo hayo Simba chini ya Phiri ilijiwekea rekodi ya michezo 3 pointi 3.
Hata hivyo rekodi haikudumu kwani iliivunja na kuweka rekodi nyingine ya michezo 4 pointi 4, rekodi ambayo ilikaa kwa muda wa siku 6 tu na siku ya 7 ikavunjwa na kuwekwa rekodi nyingine mpya na kali zaidi ya
Michezo 5 - Sare 5 - Magoli ya kufunga 5 - Magoli ya kufungwa 5 - Point 5. Unaweza kukong'oli hapa kwa taarifa zaidi:
League Rankings | The Official Website of Azam Football Club
Hakuna shaka hatima ya Phiri sasa iko mikononi mwa kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime ambaye timu yake itakutana na Simba tarehe 1 Novemba 2014 katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mtibwa hadi sasa haijapoteza mchezo wowote kama ilivyo kwa Simba. Hivi sasa Simba imewasimamisha nyota wake 3 kwa makosa ya utovu wa nidhamu. Endapo Simba itachapwa na Mtibwa Sugar hali itaendelea kuwa tete katika mtaa wa Msimbazi ambapo safari hii rungu litamshukia Phiri kwa kushindwa kufikia malengo aliyowekewa ndiposa nasema 'Maxime mhurume Phiri'.