๐— ๐—˜๐—ง๐—” ๐—ธ๐˜‚๐—ณ๐˜‚๐—ป๐—ด๐—ถ๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ ๐˜‡๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ๐˜๐˜‚๐—บ๐—ถ๐—ฎ๐—ท๐—ถ ๐˜„๐—ฎ ๐—ช๐—ต๐—ฎ๐˜๐˜€๐—ฎ๐—ฝ๐—ฝ

The thinker27

Senior Member
Sep 15, 2023
123
131
๐—›๐—ฎ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ๐—ป๐—ถ ๐˜‡๐—ฎ ๐—บ๐˜‚๐—ฑ๐—ฎ ๐—ต๐˜‚๐˜‚ ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐˜‚๐˜‚!

Natumai asilimia kubwa mtakuwa mmeshuhudia wimbi kubwa la watu wanaolalamika kufungiwa namba zao za Whatsapp kutokana na kutotumia Official Whatsapp App


Watumiaji wengi wa Whatsapp mbalimbali zisizo rasmi kama vile GBWhatsapp , YoWhatsapp, FMWhatsap n. k wamekuwa wakifungiwa namba zao permanently


Swali ni kwamba je ni kwa nini META ambao ndio wamiliki wa Whatsapp wanashindwa kuzifungia hizo Unofficial Whatsapp na badala yake wanawaumiza watumiaji wake ambao pengine walikuwa hawana uelewa wa kutosha ama walifuata features ambazo kwao wanaona ni bora kuliko zilizopo Official Whatsapp kama vile kupost status ya mpaka 45 sec, kuview deleted messages and statuses , ghost mode , flight mode n.k


Pia META nazani wanatambua uwepo wa hizi features ambazo zinawafanya watu watumie hizo Unofficial Whatsapp , je META ina mpango gani wa kuweza kuongeza baadhi ya features katika Official Whatsapp ili kuvuta wateja zaidi ?


โœ๏ธโœ๏ธโœ The thinker27
 
Mimi sidhani kama META wamekosea kufungia direct watumiaji tofauti na kufunga Servers za hao YoWhatsApp FMWhatsApp na GBWhatsApp n.k Kwa sababu walishatoa announcement kuhusu hao wanaotumia unofficial WhatsApp so ilikua ni mteja mwenyewe amue basi mwenyewe...ikumbukwe kama kutakua na Data Leakage Hizi Unofficial WhatsApp hawatakua responsible badala yake malalamiko yataenda direct kwa META maana hao wamiliki wenyewe ni Ghost
 
Hawana uwezo wa kuwafungia ni app undawnload kusikoeleweka Meta watafungia nini? Pia META sio kwamba hawana uwezo wa kutengeneza hizo feature ni kwamba hawataki kutokana na malengo yao ya biashara na kama hizo feature ni kweli nzuri na zinawalinda watumiaji wote.
 
Pia nadhani kwa kiasi fulani hawawezi kuwafungia namba kwa kudumu kwa kuwa namba zinakuwa recycled namba unayopata leo ukinunua SIM kuna uwezekano mkubwa ishatumika na mtu mwingine kwa hiyo kama hiyo ban ni ya kudumu itaathiri asiyehusika, nadhani wanaweza kupiga ban miezi kadhaa labda.
 
Msaada wazee, namimi nmetumiwa notisi kuwa sio mda wataban namba yangu nayotumia kwenye yowhatsapp. Shida Iko hapa Sasa..Whatsapp official nliacha kuitumia baada ya kuwa nimesahau 'security pattern' Sasa napotaka kuirudia inadai zile pattern, na hata nikipress 'forgot password' inadai 'middle name' ambalo nikipress inasema sio Jina sahihi.
Nafanyaje hapo wazee!!?
 
Nadhani hawawezi kuzifungia kwa sababu hizo unofficial zinatumia serve ya official wasap Ila wao wame-modified tuu.

Mm mwanzo nilikuwa natumia GB wasap kwa sababu ya kuview status/jumbe zilizofutwa tofauti na hvy nlkuwa sina tofauti na anayetumia wasap ya kawaida.
 
Hivi server ununue wewe ulinzi uiwekee wewe halafu mwingine aje achomeke ka app kanako fanana na app orijino. Wewe mqenye app orijino unatuhakikishia vipi kuwa data zetu ni salama? Ikiwa tu server zako kuna mtu anaingia na kutoka na anazidi kupata watumaaji wengi? Wataalam hii imekaaje?
 
Mi mwenyewe wanentumia hlo onyo ya kubadili ila nmekausha je huwa Wana ban number au hyo app wanaizuia isifanye. Kazi
Kama hiyo namba unaitegemea sana ,Futa hiyo whatsapp unayotumia then pakua Official whatsapp kutokea google play haraka kabla hawajafanya yao
 
META Hospitali huduma mbovu sana, wanahangaika na mambo ya Whatsapp
META Mbeya sio!!?
Mi' nina line mbili. Moja, nilikuwa naitumia kwa "Yowhatsapp" na nyingine "official Whatsapp".Cha kushangaza, hiyo Official, ndiyo imefungiwa. Tena wananiambia nitumie official, na download upya kupitia play store, bado inagoma, na kuambiwa nitumie official!
Lakini nikiweka namba ambayo haijatumika kwenye Whatsapp inakubali. Ni kama vile, wametuchoka, na sasa wanawataka watumiaji wapya!
 
Back
Top Bottom