Mbona habari za vurugu ni kila upande. Mtoa uzi anasema CCM imejiandaa kufanya vurugu nami nimesikia wafuasi wa CCM wakisema CDM wamejiandaa kufanya vurugu pindi mgombea wao akishindwa. Kwamba wataifanya Meru isitawalike. Yote hayo ni tetesi hakuna kilichothibitishwa. Ila kama wahenga walivyosema lisemwalo lipo kama halipo laja; basi ni wajibu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuna ulinzi na usalama wakutosha ili Arumeru isije kuingia katika historia ya vurugu za baada ya uchaguzi - PEV isj