Jamaa mmoja aliyekuwa ameng'oka meno kadhaa alishauriwa na rafiki yake kuwa akienda zahanati fulani ya meno basi ataweza kuwekewa meno mengine, na ndipo siku moja akaamua kwenda kwenye hiyo zahanati na Maelezo kati ya yeye na daktari yakawa kama ifuatavyo;
Jamaa: habari daktari!
Daktari:nzuri nikusaidie nini?
Jamaa: Nimeng'oka meno kadhaa na nimesikia kuwa hapa mnaweza kuniwekea meno mengine.
Daktari:Yah! Ni kweli kama umeng'oka meno hapa huwa tunakuwekea meno mengine ya bandia.
Jamaa:Haa! kweli tunakoelea sasa siko vitu feki vya kichina hadi kwenye afya si mtatuua sasa kwani original hayapo hadi uniweke ya bandia!?
Daktari akabaki hoi asijue amjibu nini mteja wake. Hii imetokea kweli wiki iliyopita hapa Dar.