Members wengi wa JamiiForums ni watumiaji wa Tecno

Mimi ni mpenzi wa teknolojia mbalimbali.Labda niwaambie wale anti-tecno.

Tecno brand ni nzuri kwa basic function za simu ambazo ndio wengi wetu tunazitumia kila siku mf.kupiga,kutuma meseji na kuperuzi mitandao ya kijamii. Sidhani kama haya pekee yanahitaji mtu awe na iphone 7 ama Samsung S7!

Naongea nikiwa mmoja ya watu waliowahi kutumia hizo simu na sikukumbwa na tatizo lolote so far.

Kiukweli Tecno ziko njema in-terms of perfomance on the basics hasa katika utunzaji wake wa charge, ukizingatia kuwa kipindi wanaanza tu na smartphone zao makampuni mengi makubwa yalikuwa hayafui dafu katika hilo.

Kabla yao ilikuwa ili umalize siku lazma kuicharge android yako mara 3-5 kwa siku na hio ni katika heavy usage, tatizo likazidi hadi yakaletwa ma power bank yale. Mfano mzuri ni zile htc za mwanzo sense,desire na Galaxy s,ace, pocket n.k

Ila baada ya tecno kuja na N na P series tukazitumia hali ilikuwa tofauti. You would last up to 7 hours on a single charge on heavy usage. Kwa siku ukachaji mara 2 tu. Siku usipoichezea kabisa inakufikisha hadi masaa 12. That was somewhere 2009-2011.
So walishatengeneza legacy na sasa wameimarika maradufu katika hio sector unaweza pata up to 10+ hours on heavy usage katika matoleo yao mengi ukiachilia zile L series zinazokupa 12+ hours of heavy usage.

Ni baada ya muda sana ndio kampuni kubwa zikagutuka kuwa zinapigwa bao kisa battery efficiency mbovu. Nakumbuka 2013 ndio wengi waliamka kuwa a smartphone is also about battery power. Mapinduzi yakianzia kwa Sony, Lenovo, Motorola na brands nyengine zikafata tokea hapo ndio walau android zinazovumilia charge zikaanza kutufikia mtaani ila tecno walishakuwapo vyema zaidi.

So watu wanaosifia tecno musiwabeze, they are also satisfied customers ambao naamini portion yao walishatumia brand names kubwa za awali wakaona tofauti katika kukidhi haja zao za kimatumizi.

Mi siwezi kuwa biased kuacha ku acknowledge ukweli. Elewa!!!
Unaongea kisayansi, mtu hata hajawahi kutumia anaishia kuiponda tu

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Infinix, tecno, Intel wote baba yao mmoja kutoka hong kong

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app

Samahani ndugu, Mimi naomba kufahamishwa hizo tecno very classy Kuliko samsung
3tu!
 
Nipo apa mr tecno kwan nyinyi mnataka tutumie simu gani

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Unaongea kisayansi, mtu hata hajawahi kutumia anaishia kuiponda tu

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app

Pole! Tecno ni bora simu tu ambazo wachina waliamua wawaletee sababu mnapenda mambo makubwa uwezo hamna
Nilishasema hapo awali kutumia tecno wala si dhambi!
Ni uwezo wetu ulipofika
Kwani mbona hata mbuzi anakula kutokana na urefu wa kamba yake.
Ila mambo ya "sizitaki mbichi hizi ndiyo nayopinga"
Unasemaje samsung na iphone mbaya na unatumia simu ya laki 2 ambayo huwenda huko Samsung au iphone ndio simu za bei rahisi sana??
Ni kweli kweli Samsung na Iphone wanasimu mbaya au uwezo wa kununua yenye quality zaidi kutoka kwao huna?
 
Phantom series ndugu embu cheki bei zake

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Mimi huwa nawambia wachague wenyewe, simpelekei mtu kitu kwa kumchagulia, mwenye kuchagua SONY Experia sawa, mwenye Samsung sawa, mwenye IPhone sawa, nawapelekea tu, au wakija huku nawanunulia nawapa wanarudi nazo huko.

Ni vitu vya kawaida tu, given kwamba mtu anakuwa na uwezo wa kuzinunua hizo kumi kwa mpigo na kuzigawa kwa wanazotaka bila kufanya biashara.

Nimerudi bongo airport na mabegi yamejaa zawadi nawambia customs hizi zawadi wamekataa, wamesema wewe lazima utakuwa unafanya biashara. Zawadi haziwezi kuwa nyingi hivi.Nawaambia sasa nimekaa Marekjani nyundo kumi, passport hii hapa, mnataka nije kitoto? Wamekataa. Sijauza hata kitu kimoja. Kuja kufanya hesabu likizonzimapamojana airfare zawadi etc imeni cost karibu $20,000.

Watu sasa hivi tunaongelea real estate in major cities of the world.

Halafu unakutana na mtu anaanza habari za kuringishiana simu.

Kachelewa sana maisha haya huyu.

Watu tunatafuta satellite phone yeye anaongea habari za Samsung/Iphone/Tecno ?

Watu tunaangalia habari za deal za kiwanda cha simu, yeye bado anashobokea simu?
inabidi muanzishe jamii forum ya wenye simu zenu

sie team makapuku

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
Pole! Tecno ni bora simu tu ambazo wachina waliamua wawaletee sababu mnapenda mambo makubwa uwezo hamna
Nilishasema hapo awali kutumia tecno wala si dhambi!
Ni uwezo wetu ulipofika
Kwani mbona hata mbuzi anakula kutokana na urefu wa kamba yake.
Ila mambo ya "sizitaki mbichi hizi ndiyo nayopinga"
Unasemaje samsung na iphone mbaya na unatumia simu ya laki 2 ambayo huwenda huko Samsung au iphone ndio simu za bei rahisi sana??
Ni kweli kweli Samsung na Iphone wanasimu mbaya au uwezo wa kununua yenye quality zaidi kutoka kwao huna?
Nilikuwa natumia Sony z2, mbona sioni tofauti na hii tecno, kikubwa ni ubora picha ndio Sony niliona wako vizuri, walianza na Africa, sasa hivi wamefika India, mid east, halafu pia zimepitishwa na tbs sio kwamba wamefika kienyeji huku kwetu

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa natumia Sony z2, mbona sioni tofauti na hii tecno, kikubwa ni ubora picha ndio Sony niliona wako vizuri, walianza na Africa, sasa hivi wamefika India, mid east, halafu pia zimepitishwa na tbs sio kwamba wamefika kienyeji huku kwetu

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app

Unajua kujifariji wewe!!

hiyo siyo historia ya tecno embu itafute vizuri
 
Phantom series ndugu embu cheki bei zake

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app

Phantom ndio simu bora na gharama zaidi kutoka tecno na ndio mnajivunia??
Okay inauzwa laki6.
Samsung kuna A series,
Jseries
Sseries
Note

Kote humo hamkai kwa hiyo phantom

Sasa huko tecno J7prime tunaiweka na Phantom?
S8 tunaiweka na Phantom?
A9 tunaiweka na Phantom?
Note 5 tunaiweka na Phantom?

Na zote hapo hakuna Chini ya laki 6
Kubaliana na hali tu ndugu
Usingizi wa Serena hotel unaraha yake si sawa na wa gongazote lodge
 
Back
Top Bottom