Membe namkubali lakini nayaogopa ya Lowassa

Membe namkubali lakini nayaogopa ya Lowassa

pagalwema

Senior Member
Joined
Sep 17, 2018
Posts
102
Reaction score
138
Aman ya bwana iwe nanyi

Hali ya uchumi ngumu tujitahidi kupunguza matumizi yasio ya lazima

Membe nakukubari nafikia hatua ya kuwaza uhame chama ingawa umefutwa uwanachama bado na amini wewe una mapenzi na chama gani

Sio mbaya ukatafuta chama chochote nikupe Kura yangu

Unanikosha na misimamo yako na jinsi unavyojiamini

Lakini kwa chadema naomba aendelee kuwa lisu kwanza anaweza pili kulipa fadhila

Ingawa naona Kama membe ana mtaji mkubwa wa watu

Yaani ata sielewi, ningeshauli membe ahamie chadema shida lisu litafanywa kosa Kama la silaa

#nimekulupuka usingizini
 
Mkuu 'Pagalwema', naunga mkono hoja yako, lakini nataka niifafanue kivingine, pengine nawe utanielewa kama nilivyokuelewa wewe.

Ni hivi, watu kama Membe (naamini kwa dhati kabisa kuwa huko ndani ya CCM sasa hivi wapo wengi).
Hawa watu wamechukizwa na mienendo ya utawala wa chama chao chini ya mweyekiti wao, lakini hawana namna yoyote ila ya kuumia ndani kwa ndani wasiseme chochote kwa kuogopa yaliyowapata baadhi yao kama akina Kinana, Nape, Makamba n.k..

Hawa wtu wamo humo ndani ya CCM sasa hivi. Pangetokea jasiri wachache wakaanza kuitikisa CCM, hapo ndipo ungeona umati wa wanachama hawa wanaoumia kimyakimya wakiwa huko huko ndani.

Kwa bahati mbaya sana, huko CCM hakuna jasiri sasa hivi. Wanaokaribia sifa hiyo ni kama huyu Membe tunayemjadili hapa. Kwa bahati mbaya sasa yupo nje ya chama, kwa hiyo kelele zake hazitikisi chochote tena huko ndani kwa ndani ya chama.

Sasa dhana yangu ni hii. Hawa watu, akina Membe na wengine wasio na ujasiri lakini wana machukizo yanayowaumiza ndani ya chama chao, hwa wanatakiwa watafutwe na vyama vya upinzani wafanye kazi pamoja.

Hailazimu, na kwa kweli haifai akina Membe waingie kwenye upinzani kwa kutafuta nafasi za uongozi.

Wao wanatakiwa kufanyia kazi upinzani bila ya ahadi yoyote ya kupewa nafasi yoyote ndani ya vyama hivyo.

Kazi zao zikishaleta matokeo mazuri, basi wanastahiri kufikiriwa kuwa katika safu ya viongozi ndani ya vyama hivyo.

Maana yangu ni kwamba, kazi kwanza, kula bata ni baada ya kazi na matokeo kuonekana.

Hivi ndivyo ninavyofikiria ingetakiwa iwe mkuu wangu 'Pagalwema'.

Sasa sijui unalionaje wewe hili.

Nina hakika usingizi utakuwa umekutoka.
 
Watu wengi hawajui kuwa membe hajafukuzwa uanachama!!yale ni maazimio ya kamati!sio hitimisho bado hajapewa barua rasmi ya kumfukuza uanachama!hadi sasa membe ni mwana ccm wa kama kawaida!!!
 
Back
Top Bottom