Meli mpya kunufaisha Kanda ya Ziwa

Meli mpya kunufaisha Kanda ya Ziwa

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555
1124324


WANANCHI wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera na mikoa ya jirani inayozunguka Ziwa Victoria, wanatarajia kunufaika na meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo.
Mbali na meli hiyo mpya, meli nyingine ya MV. Victoria inafanyiwa marekebisho na itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 hadi 4,000 na tani za mizigo 200 na kurahisisha usafiri kwa wakazi hao.

Kaimu Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Geofrey Lwesya, aliyasema hayo kwa waandishi wa habari juzi walipotembelea bandari hiyo ili kuona miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA).

Alisema ujenzi wa meli hiyo unatarajiwa kukamilika Septemba mwakani na itasaidia kuongeza mapato katika bandari ya Bukoba ambayo licha ya kutokuwapo kwa meli za abiria, yamefika Sh. milioni 60 kwa mwezi kutoka Sh. milioni 29 miaka ya nyuma.

"Mwezi Septemba mwaka 2020, tunatarajia meli hii mpya itakuwa imekamilika ambayo itarahisisha usafiri kwa abiria na mizigo yao. Meli nyingine ya MV. Victoria nayo inaendelea na marekebisho ikikamilika itasaidia sana usafiri katika bandari hii na zote zitasaidia kuongeza mapato," alisema Lwesya. Kwa mujibu wa meneja huyo, bandari hiyo inatekeleza miradi mbalimbali ikiwamo ukarabati wa jengo la abiria la kisasa na ujenzi wa ofisi inayogharimu Sh. milioni 143.8.

"Baadhi ya majengo muhimu yakiwamo majengo ya abiria, sehemu za kuhifadhia mizigo, vyoo vya kisasa, vibanda vya walinzi na zote vyenye ubora wa kisasa yapo katika hatua za mwisho na Pia alisema mbali na boti ndogo zinazosafirisha abiria katika bandari hiyo, kuna meli ndogo maalumu zinazohifadhi ubaridi kwa ajili ya kubebea samaki kutoka visiwani na kupelekwa viwandani.

Aidha, alisema makusanyo katika bandari hayo yanatokana na wafanyabiashara wakubwa wanaotumia bandari hiyo ikiwamo wanaotoa bidhaa Uganda na Kiwanda cha Sukari cha Kagera (Kagera Sugar) ambaye ndiye mteja mkubwa. Kwa upande wake Mkuu wa Bandari hiyo, Bulenga Ndaro, alisema meli ni usafiri muhimu unaotegemewa Bukoba, hivyo kusimama kwa huduma hiyo kumesababisha adha kwa watu wengi.

Alisema kwa sasa bandari hiyo ambayo inahudumia visiwa viwili vya Kerebe na Gozba, haina meli ya abiria bali wanategemea boti kwa ajili ya usafiri.

"Zamani kulikuwa na meli mbili za mizigo, lakini sasa kuna meli tano kubwa zinazoingia kwa mwezi mizigo mbalimbali ikiwamo vifaa vya dukani wa tani 200 mkubwa ukiingizwa na Kiwanda cha Kagera Sugar ambao ni tani 3,500," alisema. Kwa upande wake, nahodha wa meli ya MV Luxury II, Peter Hiza, alisema anapata huduma nzuri ikiwamo kupakia na kushusha mzigo kwa wakati muafaka.

Alisema meli yake imeingia ubia na Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) kutoa na kupeleka Bukoba kutoka Mwanza. "Tunatumia bandari za serikali kutokana na gharama za kawaida na huwa nakuja Bukoba mara mbili kwa mwezi kuleta mzigo," alisema. Naye Mwakilishi wa Kagera Sugar, Shamsa Mohammed, alisema meli mpya kubwa kwa sababu kuna unafuu mkubwa katika usafiri wa njia ya maji kuliko barabara katika kusafirisha sukari. "Tani tunazosafirisha kutoka Bukoba kwenda mikoa mingine tunatumia meli kwa sababu ina gharama nafuu na inafika salama," alisema.
 
Abiria 1,200 hadi 4,000!? Haya makadirio sijayaelewa kabisa, na ajali zitazidi kuua watu wengi kwa uzembe wa makusudi.

Hiyo MV Victoria tangu ilivyokosakosa kuninywesha maji hata kwa upanga hunipandishi. Safari za majini ni risk sana aisee dah!
 
Abiria 1,200 hadi 4,000!? Haya makadirio sijayaelewa kabisa, na ajali zitazidi kuua watu wengi kwa uzembe wa makusudi.

Hiyo MV Victoria tangu ilivyokosakosa kuninywesha maji hata kwa upanga hunipandishi. Safari za majini ni risk sana aisee dah!
Ila report zinasema ndo more safe.kuliko nyingine zote.
 
Ila report zinasema ndo more safe.kuliko nyingine zote.
Kuwa salama zaidi hakumaanishi sio hatari, bali ndiyo yenye afadhali ukilinganisha na hizo zingine.

Lakini kwa ujumla safari za majini bongo ni shida tupu. Safari ikishaanza ni Mungu tu ndiye wa kumuomba aweke mkono wake. Meli hizi za serkali huwa zimechoka sana! Kuna meli nyingine ndogo ya serikali inatoka Mwanza mjini kwenda Ukerewe, ukiona imeng'oa nanga unabaki unamuomba Mungu aifikishe salama angalau kwa safari hiyo. The same to Victoria.
 
Kuwa salama zaidi hakumaanishi sio hatari, bali ndiyo yenye afadhali ukilinganisha na hizo zingine.

Lakini kwa ujumla safari za majini bongo ni shida tupu. Safari ikishaanza ni Mungu tu ndiye wa kumuomba aweke mkono wake. Meli hizi za serkali huwa zimechoka sana! Kuna meli nyingine ndogo ya serikali inatoka Mwanza mjini kwenda Ukerewe, ukiona imeng'oa nanga unabaki unamuomba Mungu aifikishe salama angalau kwa safari hiyo. The same to Victoria.
Sawa nadhani watajifunza Kwa makosa waliyoyafanya


Hiyo meli inayotengenezwa wajitahidi wasifanye makosa kama waliofanya mv bukoba meli iliegemea upande

Sent from my Nokia 1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom