dangadunguri
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 1,276
- 1,307
Picha hii niya mdogo wetu anaitwa Amina Ally Salehe, ni mkazi wa Kigogo karibu na Msikiti wa Shia, polisi post.
Ndugu yetu huyu alipata matatizo ya kuugua na wakati mwingine akili zinachanganyika kwa kiwango kidogo si kuchanganyikiwa kabisa.
Amesoma community health, chuo cha Bumbuli Lushoto na kamaliza mwaka jana 2016.
Leo mida ya mchana ametoka nyumbani hapo kigogo bila ya watu kuwa na raarifa, ila alimwambia mdogo wake ampe pesa iliyokuwabaki wakati wakitoka hospitali. Kweli alimpa na akaingia ndani, akabeba simu yake akaondoka.
Watu kuja kustuka haonekani, dogo alivyoulizwa akajibu nilimpa chenchi nikidhani anaenda kununua vocha. Huo ndio uliokiwa mwanzo wa safari yake yakutokomea kusiko julikana. Hiyo ilikiwa muda wa saa sita mchana.
Ripoti imetolewa polisi ila wamesema wao hawawezi kulifanyia kazi swala hilo hadi masaa 24 yapite na sisi ndugu zake tushindwe kabisa kumpata, ndio wao wataanza kazi yao (hatari sana).
Ndugi zangu tunawaomba kila atakayemuona huyo binti atusaidie. Hadi naandika uzi huu bado hatujafanikiwa kumpata.
0717 929 522/0712 959 630/0684043500. Hizo ndio namba za mawasiliano kwa atakayejaaliwa kupata taarifa yoyote