Lakini twende mbele na kurudi nyuma ili kuweka kumbukumbu sawa. Iringa ni kati ya sehemu chache duniani iliyoingia kwenye rekodi ya mapambano ya kidemokrasia kwa ushahi wa kuuawa mwandishi wa habari akihoji juu ya haki na usawa kwa viongozi wa dola.
Hili la Msigwa ni kutaka kutumia kodi zetu vibaya kwani hakuna kosa alilotenda moja kwa moja na hata ushahidi ni dhaifu. Ni kwanini wanasheria wakubali kupoteza nguvu na muda kwenye mashauri yasiyokuwa na maslahi kwa umma?
Hebu busara ya kawaida tu itumike kuona jinsi ya vyombo vya dola kutumika pasipo mashinikizo ya kina Lukuvi, Nape na Mwigulu ili wasiivuruge amani na waache tamaa ya madaraka kwani si lazima kuongoza watu wasiohitaji uongozi wako.
Na vyombo vya dola viwe vinabalance siasa ili kuleta fairness badala ya kutumika kwa chama fulani..