Mchungaji Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumbaka na Kumlawiti Mtoto

McCain

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
1,169
517
1b743ccd176827bd7b247c5ac638a1e3.jpg

Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Ipagala Manispaa ya Dodoma, Joshua Warioba, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Tukio hilo linaripotiwa kutokea Machi 2, mwaka huu, majira ya jioni katika kituo cha chekechea cha Efretha English Medium Pre & Primary School, kinachomilikiwa na mchungaji huyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Lazaro Mambosasa, alisema kuwa Mchungaji huyo anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuingilia mtoto huyo kila siku alipokuwa akienda masomo ya ziada (tuition) na jalada la kesi hiyo lipo kwa mwanasheria wa serikali ambae muda wowote atapeleka hati ya mashtaka polisi ili afikishwe mahakamani.

Mama wa mtoto huyo anasema kuwa alimwandikisha mwanae kusoma chekechea katika shule ya kanisa hilo Februari 2. Baada ya mdogo wake kuja nyumbani kwake na kuuliza kama mwanae nae huwa anahudhuria masomo ya ziada na kujibiwa kuwa hajui kama kuna masomo hayo. Ndipo alipoamua kufuatilia kwa majirani wengine pia kuubaini ukweli.

Walipomuuliza mtoto huyo alisema japo kwa woga vitendo alivyokuwa akifanyiwa na mchungaji huyo. Ndipo walipoweka mtego na kumfuma mchungaji huyo akiwa na mtoto huyo kwenye chumba huku nguo zake za ndani zikiwa zimeshushwa.

Wananchi walikusanyika wakitaka kumpiga mchungaji huyo lakini aliokolewa na mwanajeshi mmoja na kukimbizwa polisi.

Baada ya mzazi huyo kufika polisi aliandikiwa mtoto aende kupimwa hospitali na majibu ya daktari yalionyesha kuwa mtoto ana michubuko. Alipoulizwa mtoto huyo alisema kuwa mchungaji alikuwa akimbaka kila alipoenda kusoma.

Kamanda Mambosasa aliwataka wazazi kutowaruhusu watoto kwenda kusoma masomo ya ziada (Tuition) pasipo kuwa na uangalizi wa karibu na pia aliitaka jamii kuendelea kupiga vita dhidhi ya matendo ya udhalilishaji kwa kutoa taarifa ili hatua za kisheria zichukuliwe.
 
Nimekuja mbio nikadhani ni yule wa ufufuo na uzima.

Ila wachangiaji wa siku hizi bure kabisa.
Unakuta kondoo amenona kuliko wa nyumbani kwako what do you expect. Tafsiri sahh si kwamba mchunga kondoo amebaka ila alichinja kondoo ambaye bado hajafikia au ambaye yuko chini umri wa kufikia kuchinjwa

Kama unaifaham tasfida utakuwa umenielewa hapo
 
Huyo mchungaji inavooneka ndo tabia yake aliwahi kufanya hvo kwa mtoto wa mpangaji wake na kuna tetesi mwanawe wa kwanza ndo kamgeuza mke baada ya mke kuamua kutengana nae lkn si kwa kupeana talaka kutokana na tabia zake hzo.mwanangu pia anasoma hapoa na nafikiria kumuhamisha kwa kweli.hyuy jishua si mtu mzur kabisa.
 
Na huyo mwanao usikute keshajiolea
 
Heshima ya cheo cha uchungaji, nabii,mtume na hata askofu imeharibiwa sana na haya madhehebu ya kilokole.
 
Mchungaji wa hivyo ...unakuta ndo michezo yake kwa waumini....lakini kabainika....
 
wachungaji wa kilokole shida sana
Ni wana shida sana kuliko mnavyo wafikiria. Ni hatari wana hawa wachungaji. Kwanza wanapenda sana pesa na ni wacheza mazingaombwe. Ni wakatili sana.

Maaskofu wa kilokole ndio kabisa, hawafai. Siwapendi kabisa, wanachafua jina zuri la BWANA YESU KRISTO.
 
Hata Roma wanakamatwa kila kukicha.Hii ni roho ya mtu mwenyewe.Kanisa lisihusishwe na ujinga wa hawa wezi wamadhabahuni.
 
Ni wana shida sana kuliko mnavyo wafikiria. Ni hatari wana hawa wachungaji. Kwanza wanapenda sana pesa na ni wacheza mazingaombwe. Ni wakatili sana.

Maaskofu wa kilokole ndio kabisa, hawafai. Siwapendi kabisa, wanachafua jina zuri la BWANA YESU KRISTO.
Huko Dodoma, hayo maaskofu yenye tamaa na pesa, yanawasubiri wahamihaji toka Dar. Yaani, kama ni mlala hoi hawakutambui, ila ukionekana kuwa una kipato kizuri, wanaweza kukupa uzee wa kanisa.

Wana omba kwa kunena eti: mashambula mbashambulika kiki kikombualiko!!!! huku yakifikiria pesa tu. Hakuna cha kunena zaidi ya kumkufuru MUNGU wetu. Mikutano yao wakikutana wao kwa wao wanashambuliana kupigania milo na sio neno.

Angalia wengine wanapinga shughuli za kuzuia madawa ya kulevya, wakati wote wao ni kuzungumza kama yupo kwenye ngoma ya nanii huko pwani. Eti naye ni askofu. Wengine kwa viroba ndio usiseme, hata jana nasikia huko Songea alipata misahibu ya kulamba kiloba.
 
Ukatili wa aina hii binafsi siwezi kuuvumilia yaani ni ukatili wa aina hii utaonifanya mimi binafsi Nim Duterte!!
 
Huko Dodoma, hayo maaskofu yenye tamaa na pesa, yanawasubiri wahamihaji toka Dar. Yaani, kama ni mlala hoi hawakutambui, ila ukionekana kuwa una kipato kizuri, wanaweza kukupa uzee wa kanisa.

Wana omba kwa kunena eti: mashambula mbashambulika kiki kikombualiko!!!! huku yakifikiria pesa tu. Hakuna cha kunena zaidi ya kumkufuru MUNGU wetu. Mikutano yao wakikutana wao kwa wao wanashambuliana kupigania milo na sio neno.

Angalia wengine wanapinga shughuli za kuzuia madawa ya kulevya, wakati wote wao ni kuzungumza kama yupo kwenye ngoma ya nanii huko pwani. Eti naye ni askofu. Wengine kwa viroba ndio usiseme, hata jana nasikia huko Songea alipata misahibu ya kulamba kiloba.

Kama nasema uongo, ulizeni wanapokaa hao maaskofu. Wana magorofa na magari ya kifahari sana.Yaani ni matajiri wa kimwili kuliko kiroho. Misa zao zimetawala kuhusu kimwili tu. Mifano: kuombia utajiri wa hapa duniani, eti kapata mchumba na mibaraka ya hapa duniani tu.

Tizama mabango ya matangazo yao au kalenda, utachoka kabisa. Mipicha yao wenyewe na maneno ya kujisifu sana eti Dr. mtume, nabii, askofu ........nareefu na ujumbe we kumwili tu.

Wanapenda kuhubiri kwa namna ya kujengo hofu, vitisho ili mtoe pesa kwa woga na wao wabugie, badala ya kujenga hofu ya kuacha dhambi na kumrudia Mungu.

Tumezingirwa na watu wa maajabu sana. Wanajenga majengo makubwa ya kanisa, huku roho za watu zina nyufa. Hakuna upendo, hakuna haki, wafuta bangi wauza madawa, makahaba, ndoa zinavunjika, watoto wa mitaani kuongezeka... wao hawajui hayo. Hawasaidii hata wajane, wazee zaidi ya kuombea utajiri wao tu.

Makanisa ya leo, sio makanisa. Ni magulio tu. Eti michango ya kumnunulia gari mchungaji, kumjengea nyumba wakati yeye ana gorofa na ma VX, anataka na jingine.

Mizee mizima haina busara.
 
Kawaida sana kwa wachungaji wa kikristo kutafuna kondoo zao.

Wala sishangai.
 
Back
Top Bottom