Mchumba angu yuko Finland!

vukani

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2009
Posts
244
Reaction score
166


Naelekea Uzeeni sasa!

Ni miaka 16 sasa tangu nifahamiane naye, alikuwa ndio kwanza amemaliza kozi yake ya uhasibu na kuajiriwa katika taasisi ya misaada ya mmojawapo ya nchi za Ulaya hapa nchini.

Alipoanza kujitegemea, alipata nyumba iliyoko jirani na nyumbani kwetu, na huo ukawa ndio mwanzo wa kufahamiana naye. Alikuwa akijiheshimu sana na hakupenda kujichanganya na watu. Alitumia muda wake mwingi nyumbani kwake na kama akiamua kutoka mara nyingi alipenda kuwatembelea ndugu zake a marafiki zake waishio maeneo ya mbali.

Nilibahatika kufahamiana naye wakati fulani ilipotokea shida ya maji, na kwa kuwa, nyumbani kwetu kulikuwa na kisima, alikuja kuomba msaada wa maji na huo ukawa ndio mwanzo wa kufahamiana naye.

Naam, urafiki wetu ulimea na kukua, kiasi kwamba tulikuwa tukitembeleana mara kwa mara, alitokea kufahamiana na wazazi wangu pia na walimkubali sana, kutokana na jinsi alivyokuwa akijiheshimu.

Jambo moja lililonishangaza, ni kwamba sikuwahi kumsikia akizungumzia juu ya mahusiano yake, nilishikwa na udadisi na siku moja nikamuuliza kama anaye mchumba. Alinijulisha kuwa mchumba wake yuko Finland kwa masomo, nilimdadisi zaidi kama yuko huko kwa muda gani, akanijibu kuwa ni miaka miwili sasa. Alinijulisha kuwa mchumba wake huyo anasoma kule na itamchukua miaka 3 hadi kumaliza masomo yake na ndipo atarejea nchini na kuungana naye.

Ukweli ni kwamba rafiki yangu huyu alikuwa akifuatwa na wanaume wengi tu tena wa kutosha wakitaka kuwa na uhusiano naye, nadhani ni kwa sababu alikuwa ni mrembo sana, lakini alikuwa akiwakataa kwa maelezo kwamba, anaye mchumba tayari ambaye yuko nje ya nchi kwa masomo.

Nilimuheshimu sana kwa msimamo wake. Mwaka uliofuata binti yule alihama katika nyumba ile na kuhamia maeneo ya Sinza. Nilipoteana naye kwa takriban miaka 16. Ni hivi karibuni nimebahatika kukutana naye, alionekana dhahiri kuwa umri umekwenda.

Alinikaribisha nyumbani kwake maeneo ya Kimara, alinijulisha kuwa amebahatika kujenga nyumba yake mwenyewe. Wiki iliyofuata nilimtembelea nyumbani kwake. Alikuwa amejenga nyumba nzuri na alikuwa ameizungushia ukuta na kuweka geti. Alinikaribisha sebuleni kwake. Alinitambulisha kwa mdogo wake wa kike aliyekuwa akiishi naye ambaye alikuwa akisoma Chuo Kikuu Dodoma, na pia kwa msichana wake wa kazi.

Nilishikwa na udadisi wa kutaka kujua alipo mume wake, na labda kama ana mtoto. Alicheka sana na kisha akanishika mkono na kunipeleka chumbani kwake. Alikuwa na chumba kikubwa chenye nafasi ya kutosha na pia kulikuwa na meza kubwa ambayo ilikuwa imepambwa vizuri na vifaa vya ofisini pamoja na lap top, kwa ajili ya kazi zake.

Aliniacha kwa muda ili niridhishe macho yangu, kisha akaanzisha mazungumzo.

Mwenzangu, alianza simulizi yake, …….. Unadhani kipindi kile wakati nakwambia kuwa ninaye mchumba na yuko masomoni Finland ilikuwa ni kweli, la hasha, haikuwa kweli, bali nilikuwa nadanganya tu kwa sababu sikutaka kusumbuliwa na wanaume. Si unajua wanaume wa siku hizi wanapenda kuwachezea wanawake! Sasa mimi kwa kuliepuka hilo nikaona nitumie mbinu hiyo ili kuepuka usumbufu. Nilibaki mdomo wazi….

Basi bi dada………… aliendelea…….. nilipohama pale Mikocheni, na kuhamia Sinza, niliendelea na msimamo mwangu, sikuwapa wanaume nafasi, nilikuwa na malengo yangu na nilitaka nihakikishe yanatimia.

Ni malengo gani hayo…… nilimdadisi……

Kwanza, nilitaka nijenge nyumba yangu mwenyewe, na pia ninunue gari na kuanzisha biashara zangu na sasa nimetimiza malengo yangu, sasa tatizo linakuja.

Tatizo gani tena………..nilimuuliza.

Sitongozwi na wanaume……… na wananiogopa!..............haki ya Mungu mdogo wangu, yaani nina wakati mgumu kweli.

Mh! Niliguna…… wewe unadhani tatizo ni nini? Nilimuuliza,

Sijui sababu, lakini, naona kama vile hakuna anayevutiwa na mimi, najitahidi kuongea na wanaume lakini tunaishia kupiga stori tu, na wengine wananitongoza lakini ni waume za watu. Mwenzio naogopa kweli, mpaka nimejenga wasiwasi kuwa labda nimelogwa.

Mh……….Nilishusha pumzi……….Vumilia dada Jane, utampata atakayekufaa, muombe sana Mungu, atakupa mume aliye mwema, nilimpa moyo.

Mh, mdogo wangu, umri huu? Unajua mwakani natimiza miaka 39, mwenzio nazeeka hivyo, atanioa nani….! Nimekuwa nikibadilisha makanisa kama nini, katika kuombewa na kote huko naona maombi yangu hayajibiwi.

Marafiki zangu karibu wote wameolewa na wanaishi na waume zao, mimi tu, sijui nina mkosi gani…. Nilimuona Dhahiri machozi yakimlengalenga….

Nilimpa moyo na kumshauri asikate tamaa. Nilimwambia arudi kwenye kanisa lake la awali na ajiunge na kwaya ikiwezekana ashiriki kwenye kamati mbalimbali za kanisa na zitakazomfanya akutane na watu mbalimbali. Nilimwonya awe makini sana na wanaume walaghai kwani wapo wengine wanaweza kutumia mwanya huo kummimbisha na kumtelekeza.

Alikubaliana na mimi na tukamaliza mazungumzo yetu kisha nikaondoka kurejea nyumbani…….. mweh dunia hii……. Habari ya dada Jane si kwamba tu ilinishangaza, bali pia ilinisikitisha. Yaani zaidi ya miaka 16 aliishi kwa kusema uongo ili kuwakwepa wanaume! Alichokuwa akikiogopa kwa wanaume ni kitu gani hasa?

Nilibaki nikijiuliza maswali chungu mzima na sikupata majibu.
 
Nice!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Ndo ubaya wa kuamini kila kitu unachofikiria ni sahihi. Sometimes we have to share our feelings with our friends not necessarily to be our close friends but anyone whom you might be confortable, it helps. Asikate tamaa, bado anaumri mzuri, ila asiwe na presha sasa. She has to relax and say she can do.
 
Sasa wewe kwa tamaduni za Kiafrika wewe ni MSHAMBA...Unajua mwanamke hawezi kukupeleka chumbani kwake wakati ana vyumba vya wageni? Kwa taarifa yako ALIKUWA ANAPROPOSE wewe...
 
Mume keshapata tayari!! Nyumba na gari ndio mume wake
 
Mwenyewe aliona finland ni mbaaali au sio..nkt finland kawaida tu sasa mim sijaona point yake..ni kama vile amejinyima experience ktk tasnia ya mapenzi..over..
 
::
Maneno yanaumba
Ni kweli mumewe yuko Finland ana reseat course
Chezea supplimentary wewe!
=
 
pamoja na kuwa ni hadithi.....
huyo dada hawezi kuwa serious.....

Wanaume wote hawa waliojaa?
Wapo kibaaaaaaoooooo wanatafuta kulelewa....

Angejivutia mmoja
 
Ni Kweli wanaume wako wengi, ila husband material ndiyo hawapatikani kwa urahisi.
pamoja na kuwa ni hadithi.....
huyo dada hawezi kuwa serious.....

Wanaume wote hawa waliojaa?
Wapo kibaaaaaaoooooo wanatafuta kulelewa....

Angejivutia mmoja
 
Kamuuzie Shigongo deal hilo atunge riwaya zake atauza sana...tena aweke stori ya kweli....atauza sana!hizo zipo sana tu na zinawakuta sana wadada na hata wakaka...wengi walioko ulaya wana hayo matatizo sana ..
 
Na utandawazi wote huu wanawake wanangoja kutongozwa tu?

Hawaoni wenzake wanavyochangamkia tenda JF?

Halafu mwanamke anaweza kumtongoza mwanamme na kumfanya mwanamme afikiri yeye ndo kaanza kumtongoza mwanamke.

Story ya kutunga au mdada ana matatizo ya kisaikolojia.
 
Hii kali sana,sometimes unaweza sema kama papa aliyestaafu hivi majuzi kuwa, siku moja aliwaza huenda mungu amelala.Manake yanayotoekea duniani ni kama msimamizi kaenda likizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…