Mchina akamatwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nyerere akijaribu kutorosha meno ya ngiri

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
122,494
96,073
Wachina wanaojidai kuwa ndio wafadhili wetu wakubwa wa miradi mbali mbali hapa nchini baadhi yao wanatumia mwanya huo kutuhujumu hasa pale wanapoamua kuwa soko huru la kununua nyara za taifa letu hasa viungo vya wanyama wetu.

Jana uwanja wa ndege jijini DSM amekamatwa mchina akiwa na meno ya ngiri akijaribu kuyatorosha kwenda nayo kwao.

===============

Jeshi la Polisi la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) linamshikilia raia wa China kwa tuhuma za kukutwa na meno mawili ya ngiri anayodaiwa kuyatengeneza kama vidani kuvihadaa vyombo vya usalama.

Kamanda wa Polisi JNIA, Martin Otieno alisema jana kuwa raia huyo ni mkazi wa Guangdong alikamatwa juzi saa 7.30 mchana wakati akijiandaa na safari ya kuelekea Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Alisema polisi wa JNIA kwa kushirikiana na maofisa wa wanyamapori walitilia shaka begi lake wakati linafanyiwa ukaguzi.

Otieno alisema mtuhumiwa huyo alipokuwa anakaguliwa kwenye mashine za ukaguzi ndipo walibaini kuwa ameficha vidani vya meno hayo ndani ya begi lake dogo.

“Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika eneo la ukaguzi wa mwisho wa abiria tulipomhoji alidai kuwa vidani vya meno hayo amenunua Afrika Kusini,” alisema Otieno.

Otieno alisema mtuhumiwa huyo alidai kuwa alinunua vidani vya meno hayo kwa ajili ya urembo lakini walipochunguza hakuwa na kibali kinachoonyesha nchi aliyonunua.

Kamanda Otieno aliwaomba wananchi kuwa na uzalendo wa nchi yao wanapoona mtu anasafirisha rasilimali za nchi watoe taarifa Jeshi la Polisi.

Alisema polisi wataendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo ya mipakani na viwanja vya ndege ili kudhibiti aina hiyo ya utoroshaji wa nyara.

Otieno alisema uchunguzi unaendelea ili kumfikisha katika vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazomkabili.


Chanzo: Mwananchi
 
Hahahahahahaa walipokuwa wanajenga daraja la ruvu, nyoka wote, vyura, samaki, paka na mbwa vyote viliisha.... so huoni kwamba hawa watu sio wenyewe kabisa??
 
Yaani baada ya meno ya tembo na pembe za faru sasa wamegukia akina chekanae? mwisho binadamu tutang'olewa meno!
Daaaa wewe jamaa umenichekesha sana asubuhi hii,cheki huyo ngiri masikini na urembo wake sasa ni dili nchini kwa wafadhili
1462428357646.jpg
 
Kuna siku niliona bbc wachina wakihojiwa,wakasema demand ya meno,kucha na pembe za wanyama hawa ni kubwa nchini china kiasi kwamba hata wakipewa wanyama wote walioko africa bado hawatoshelezi mahitaji!
 
Kuna siku niliona bbc wachina wakihojiwa,wakasema demand ya meno,kucha na pembe za wanyama hawa ni kubwa nchini china kiasi kwamba hata wakipewa wanyama wote walioko africa bado hawatoshelezi mahitaji!
Duuuuuu,hapa sasa naanza kupata mwanga wa ni kwanini hawa jamaa wamekuwa na vipau mbele vya kuzifadhili miradi mikubwa nchi za afrika
 
Walipo jinasibu kama wafadhili walijua watachukua rasilimali zetu na kurejesha sehemu tu ya faida waipatayo, TZ imegeuka kama changudoa anaejiuza anajikabidhi tu kwa mteja kwa ajili ya fedha bila kujua anachoenda kukutana nacho.
 
Daaa huu mradi wa reli ya kati kuna baadhi ya misitu mikubwa na wanyama wengi sijui hali itakuwaje huko!!
 
Back
Top Bottom