Samahani sikuwa hewani jana, imerudiwa jana asubuhi kuanzia saa 4.30 asubuhihadi 4.50 ambapo matokeo yalibakia yaleyale 1-0: Kwa ujumla mchezo wa marudio ulikuwa burudani tamu kwa waliofika kushuhudia mchezo huo wa dakika 20 kutokana na speed ya mchezo na gonga za kutafuta magoli ambazo ziliishia mikononi mwa kipa wa TESSEMA Hashimu Nzota ambaye kwenye mchezo wa kiporo alifanya miujiza mingi kuiokoa timu yake kwa kuchomoa michomo 05 iliyokuwa inahesabiwa kama mabao kwa Kimondo!. Tessema wana ukuta mzuri na kipa wao ana uwezo wa kiwango cha juu kiukweli nadhani ni kipa anawezesha kuchukua nafasi kwenye timu za ligi kuu na taifa, labda kikwazo kitabakia ufupi alio nao.