Mchezaji mwingine afariki dunia Argentina

Buenos Aires

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
1,894
1,622
Mchezaji mwingine afariki dunia Argentina
Na whezron - May 24, 2016
micael.jpg_973718260-640x465.jpg


BUENOS AIRES, Argentina

MCHEZO wa soka umekumbwa na tukio jingine la kusikitisha ambapo mchezaji wa Kiargentina, Micael Favre amefariki dunia baada ya kupigwa mara mbili kichwani katika mchezo uliofanyika Jumapili ya wikiendi iliyopita.

Kabla ya kukumbwa na mauti, Favre (24) alikuwa akiichezea klabu ya San Jorge iliyokuwa ikikabiliana na Defensores katika mchezo wa Liga Departamental de Colon nchini humo.

Akiambaa na mpira pembeni mwa uwanja, Favre alisukumwa na mchezaji wa Defensores na kuanguka chini ambapo goti la mchezaji wa timu hiyo lilimgonga kichwani Favre ambaye aliamka kwa hamaki na kumlalamikia mchezaji huyo aliyemsukuma.

Wakati huo huo, mchezaji mwingine wa timu ya Defensores alijitokeza na kumpiga kichwani Favre aliyekuwa akihoji kuhusu faulo aliyochezewa, kabla ya kuanguka tena na kupoteza nguvu ya kusimama kwa mara nyingine.

Timu ya madaktari ilishtushwa na hali isiyokuwa ya kawaida ya Favre na bila kupoteza muda wakambeba kwenye gari maalumu ya wagonjwa (Ambulance) na kumpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu, lakini Favre alianza kuonesha hali ya kushtuka kila mara na kupoteza maisha kabla ya kufikishwa hospitalini.

Chanzo cha kifo cha mchezaji huyo kitawekwa wazi mara baada ya mahakama kupitia tena marudio ya tukio hilo kwenye kipande cha video na kuzungumza na mashahidi waliokuwepo wakati wa tukio hilo.

Chama cha soka nchini Argentina (AFA) kilitoa salamu za rambirambi kwa klabu yake pamoja na familia ya Favre ambayo ilisomeka hivi: “AFA inatoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Micael Favre, mchezaji wa San Jorge, kifo kilichotokea katika mchezo wa Liga Departamental de Colon dhidi ya Defensores.

“Chama pia kinachukua nafasi hii kutoa salamu za pole kwa familia ya Favre na wote waliopo ndani ya klabu ya San Jorge.”
 
Back
Top Bottom