Mchezaji apewa kadi nyekundu kwa kutoa hewa mbaya uwanjani

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Refa mmoja raia wa Sweden, alimpa kwa mpigo kadi mbili za njano mwanasoka Adam Lindin Ljung-kvist, akiwa uwanjani, kwa kosa la kutoa hewa mbaya.
Mchezaji huyo alipokuwa katika harakati za kushangaa kuhusiana na hatua ya refa huyo, alipigwa kadi nyekundu na kuondolewa uwanjani.
Refa huyo ametaja kitendo cha Adam cha kutoa ushuzi , kama tabia isiyo ya mchezaji.

Lakini kulingana na Adam, alidhani alikuwa akifanya hivyo kimaumbile tu na wala hakuwa na nia ya kumchafulia refa hewa.

Taarifa hiyo imeibua malumbano makubwa kote duniani katika mtandao wa kijamii, huku wengine wakisema kuwa hiyo ni mara ya kwanza kwa mchezaji soka kupigwa kadi nyekundu kwa sababu ya kuchafua hewa.

0


0
 
Back
Top Bottom