Mchele kutoka Mbeya

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,433
Reaction score
38,402
Ukiwa Dar es Salaam maduka ya mchele huwa yanajinadi kwa mbwembwe MCHELE SAFI KUTOKA MBEYA

Ukishafika Mbeya unakutana na maduka ya mchele yakijinadi
PATA MCHELE SAFI KUTOKA KYELA

Ukifika zako hapo mjini Kyela unakutana na maduka ya mchele nayo yakijinadi TUNAUZA MCHELE SUPER KUTOKA IPINDA

Unakufahamu Ipinda wewe? Ukishafika unakwenda zako duka la mchele. Mwuzaji anakwambia HUU NI MCHELE SUPER KABISA KUTOKA BONDE LA TENENDE

Halafu ikitokea ukazurura hadi Tenende wenyeji wanakwambia MCHELE SUPER NI ULE WA SHAMBA LA MZEE MANJOLI.

Ukifika kwa Mzee Manjoli anakwambia mchele super ni ule wa shamba la MKE MKUBWA

Unashangaa?


Kila kizuri kina kizuri zaidi yake usituletee maringo kwa uzur wako kuna wazuri zaidi Yako .......[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…