sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,687
- 1,111
Tunataka kuona katika taifa hili vijana jeuri na wenye kujiamini,si vijana waoga,akina "ndiyo bwana mkubwa",vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya kitanzania. Tunataka vijana waasi dhidi ya mifumo kandamizi,ubwana na ufisadi katika taifa.
Si maneno yangu bali ni maneno ya mpigania Uhuru na muasisi wa chama cha mapinduzi na rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hayati Julius Kambarage Nyerere. Nimeamua kusimamia maneno haya ya kunitia ujasiri toka kwa baba wa taifa hili kama sehemu ya kumuenzi na kujaribu kuishi alivyoishi yeye kivitendo kwa kuchukia mifumo inayojengwa na misingi ya kinafiki.
Kizazi hiki ni kizazi cha kuhoji kwa hoja(facts) kila panapo onekana utata na sintofahamu inayotaka majibu ya kina. Kwa kutumia hifadhi ya maneno ya Mwalimu kwa vijana wa Taifa hili nami nawajibika kuwa muasi dhidi ya mifumo kandamizi,ubwana na ufisadi katika taifa.
Leo nitazungumzia kidogo taarifa ya michango ya kufanikisha zoezi zima la kuwaaga ndugu zetu,watoto wetu na jamaa zetu waliotangulia mbele ya haki. Mazungumzo yangu yatakuwa katika mfumo wa kuhoji ili kujiridhisha kutokana na taarifa ya michango mbalimbali iliyotolewa na makundi mbalimbali.
Ni ukweli usiopingika kuwa taifa limepoteza nguvu kazi ya taifa ijayo lakini wazazi pia wamepoteza vijana wao ambao walikuwa na mategemeo nao katika maisha ya sasa na yajayo pia,ni kweli pia hakuna gharama inayoweza kuziba pengo hilo zaidi ya kufarijiana,lakini tuna haki kama wananchi kujua juu ya michango iliyowasilishwa kwa nia njema tu.
Kwanza nichukue fursa hii kuipongeza serikali kuu kupitia mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kuratibu zoezi zima la kuhakikisha vijana wetu wanasitiriwa katika safari yao ya mwisho hapa duniani,Mungu azilaze peponi roho zao amiin.
Kutokana na michango hiyo,serikali kupitia mratibu wa mazishi haya ambayo serikali imesimamia na kugharamikîa,tumesikia jumla kuu ya michango na jumla ya rambirambi kwa wafiwa na kilichobaki ndicho kilicho tumika kugharamikia shughuli nzima.
Napenda kuihoji serikali hii tukufu,uko wapi mchango wa serikali kutokana na ahadi yake ya kugharamikia shughuli nzima ya mazishi?
Ili kuondoa sintofahamu ya idadi na matumizi ya michango serikali kupitia mratibu wake ambaye ndiye mkuu wa mkoa kutoa mchanganua wa michango iliyopatikana na matumizi yake ili Watanzania wajiridhishe kuepuka sintofahamu kama ile ya tètemeko la Kagera ,haitoshi kutuambia familia za wafiwa zimepata 3.6miliioni na zilizobaki ndizo zilizotumika kwa ajili ya shughuli nzima.
Pia niikumbushe serikali kuwa inapotoa michango ijue imegusa fedha za Watanzania,hivyo ni vizuri wenye fedha zetu kufuatilia mwenendo mzima na si kujifichia kwenye michango ya wasamaria wema na kutoa maneno matupu,tuomba mrejesho.