Mbuzi kuzagaa hovyo Dar, mamlaka zipo wapi?

majebsmafuru

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2017
Posts
463
Reaction score
649
Licha ya kuzagaa ovyo wanaogopwa kuwa ukiwagusa umeumia kwa vile wanachungwa kishirikina. Ndiyo maana nachelea kusema kuwa hata serikali-Halmashauri ya Jiji na manispaa zako zinahofia kulogwa.

Mbuzi hawa wamekuwa kero kubwa barabarani kutokana na kujichunga wenyewe wanapokwenda kutafuta chakula.

Makundi haya ya mbuzi huonekana kwenye Barabara ya Bagamoyo maeneo tofauti kuanzia kituo cha mabasi cha kwa Komba.

Hatari inayoweza kusababishwa na mbuzi hawa ni pale wanapokatisha barabara huku magari yakiwa kwenye mwendo wa haraka.

Mbuzi wengine katika barabara hiyo huonekana eneo la kituo cha Africana na unapoelekea maeneo ya Tegeta, kuna kundi lingine eneo la kituo cha JKT.

Makundi haya huzagaa katikati ya barabara na kadri siku zinavyokwenda ndivyo wanavyozidi kuongezeka kwa kuzaliana.

Ukiendelea mbele kundi lingine unakutana nalo kituo cha Tegeta kwa ndevu, wakivinjari kwa kutafuna mabaki ya vyakula vinavyoteremshwa na magari katika soko la Tegeta.

Aidha, ukifika maeneo ya kituo cha Boko California, kuna kundi lingine pia linakaa barabarani likipishana na magari.

Kila siku mbuzi hao hujiongoza wenyewe kwa kuzingatia muda wa kutoka na kurudi wanakolala. Hata hivyo, haijajulikana mmiliki wa mbuzi hao katika maeneo hayo tajwa anawaache mbuzi hao wakizagaa bila kuwahifadhi kwenye zizi.

Licha ya kuonekana wakijiongoza wenyewe, hakuna mtu anayethubutu kuwagusa kwa kuwaogopa na baadhi ya watu wanaoishi maeneo hayo wanadai wanaongozwa kwa imani za kishirikina.

Imani hiyo imewafanya hata vibaka na wezi wa mifugo kuwaogopa na mbuzi hao wakiendelea kutamba barabarani.

Mifugo hii kuendelea kuzagaa barabarani inachangia uharibifu wa mazingira kutokana na vinyesi wanavyoviacha.

Vile vile wanaharibu miti iliyopandwa pembeni ya barabara na katikati ya barabara kwa kuitafuna wakati wanapotafuta chakula.

Watu wengi wanauliza mbuzi hao kweli wapo kwa imani za kishirikina na kusababisha hata mamlaka za usimamizi wa mazingira kushindwa kuwaondoa kwa kuogopa?

Mbuzi wapo sehemu nyingine za jiji hivyo ina maanisha Temeke, Ilala, Kigamboni kama ilivyo Ubungo na Kinondoni viongozi wanaogopa kulogwa ndiyo maana mbuzi hao hawaguswi.

Lakini suala la mbuzi kujichunga ni jambo linalozungumzwa katika sehemu nyingi za Dar es Salaam , mathalani hata Ubungo na Kimara wapo. Wanaachwa mitaa kwa hofu za imani za kishirikina hivi hali hiyo itaendelea mpaka lini?

Hivi ule utaratibu wa kutaifisha mifugo inayozagaa barabarani kwa kuipiga mnada umekwenda wapi? Kwa sababu hatua hiyo ingesaidia kuiondoa mifugo hiyo na kuondoa usumbufu.

Kama mifugo hiyo ingekusanywa na kupigwa mnada, serikali za mitaa husika zingejiingizia mapato kwa njia hiyo na wenye mifugo wanaoiacha ikizurura ovyo, wangeacha tabia hiyo.

Mbali na kuchafua mazingira, mifugo hiyo imekuwa kisababisha ajali madereva wanapojaribu kuikwepa.

Vyanzo vingi vya ajali zinazotokea nchini, baadhi yake zinasababishwa na mifugo kukatisha ovyo barabarani.

Tabia ya wenye mifugo kuiacha ikizagaa kwenye barabara kubwa na mitaani imekuwa ya kawaida kutokana na kutochukuliwa hatua, ikiwamo ya kukamatwa kwa mifugo yao na kutaifishwa.

Awali, mifugo ilipokutwa ikizagaa barabarani bila mmiliki kujitokeza, ilikuwa ikisombwa kwenye lori na kupelekwa jiji kwa ajili ya kupigwa mnada.

Kero hii ya mifugo kuzagaa barabarani haipo tu kwa Barabara ya Bagomoyo, bali hata barabara nyingine za mjini na ziendazo mikoani.

Sheria ndogo zilizowekwa na manispaa lazima zitekelezwe ili kuondoa kero mbalimbali zinazosababishwa na watu wachache wasiofuata utaratibu.

Aidha, sheria zinaeleza wazi kuwa sehemu ya makazi ya watu, watu hawaruhusiwi kuweka mifugo ili kuepusha bugudha kwa wengine na halafu inayotoka kwa wanyama hao.

Watu wanaomiliki mifugo wanatakiwa kutafuta mashamba mbali na mji ambako watapata sehemu nzuri ya malisho na kuwaepusha watu wengine na kero ya uchafuzi wa mazingira.

[email protected]; Simu: 0774 466 571

Mbuzi kuzagaa ovyo Dar mamlaka zinahofia kulogwa? - Mbuzi kuzagaa ovyo Dar mamlaka zinahofia kulogwa? via @Shareaholic
 
Hao siyo mbuzi ni watu(bibi zake na Bashite) jaribu kuziiba uone moto wake.
Hakuna kitu kama hicho, ukiwaza hivi hata albino waweza kuuwa kama sio kuuwa vibibi vizee kisa macho mekundu! Acheni uzuzu wa ushirikina, tunazidi kuwa maskini sababu ya mambo ya kijinga kama hayo...
 
Mi naona mbuzi kujichunga wenyewe ni nzuri tu.inaonekana wewe hujawahi chunga hata bata ni adhabu acha yajichunge menyewe.kwa suala la ushirikina mbuzi kujichunga wenyewe ni kweli kuna mbuzi mmoja huwa analiongoza kundi nahisi huyo ndo huwa kalishwa hiyo ndagu na huwa mkorofi
Na hata wengine hutiwa dawa kiasi kwamba hata mwizi akitaka kuwaiba roho yake husita na anaweza ishia hata kuwasindikiza mpaka home
Mi naona mbuzi kujichunga wenyewe ni nzuri tu.inaonekana wewe hujawahi chunga hata bata ni adhabu acha yajichunge menyewe.hakuna mnyama msumbufu machungani kama meeee huwa hatulii .kwa suala la ushirikina mbuzi kujichunga wenyewe ni kweli kuna mbuzi mmoja huwa analiongoza kundi nahisi huyo ndo huwa kalishwa hiyo ndagu na huwa mkorofi

Hao wanaitwa mbuzi wa mpemba, OGOPA
 
Ndugu dar kwa sasa kila kitu kinazagaa hadi biashara
 
Unachosema Ni sahihi kabisa Mimi naishi maeneo ya mbezi jirani na tangi bovu hao mbuzi wapo miaka mingi.Sehemu hizo mpaka kwa Londa mifugo imezagaa yaani wanaharibu mazingira na kuyachafua sana .Sehemu za wazi watoto hawawezi kucheza kwa sababu ya kinyesi Cha mifugo yaani ng'ombe,mbuzi na kondoo.Mmoja hapa jirani Ni MCCM ukienda serekali za mitaa hawafanyi chochote.Paul Makonda ,mkuu wetu was mkoa jamani tunaomba Masada wa kuwataka wafungie mifugo yao ndani jamani.Maeneo yetu Ni hapa kupandia kwa shule ya Mbezi kwa mbowe jirani na kanisa katolliki na makaburi .
 
Hata wanawake binadamu siku hizi wameamua kufyatua tu, yaani kila baada ya wanawake 3 unakutana na mwanamke kabeba kachanga, hivyo sioni ajabu!!
 
Mimi nimefanya kazi Bagiamoyo miaka4.Hao ukiwagusa Kwa lengo baya ni hatari.Wengi ni makafara na wameshasomewa.Wengine ni Wa watu wababe kishirikina.Wahuni Wa mjini unadhani hawajawaona?gusa unate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…