Mbunge wa CHADEMA amkubali Rais Magufuli

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
MBUNGE wa Jimbo la Same Mashariki, Naghenjwa Kaboyoka (Chadema) amevunja ukimya na kumuunga mkono Rais John Magufuli katika hatua yake ya kutaka kupunguza mishahara ya vigogo sekta za umma. Aidha alimtaka Rais kuzielekeza fedha nyingine katika kuboresha sekta za afya na elimu.

“Naunga mkono sana hatua za Rais, kuna sababu gani mfano watumishi wa umma kulipwa wastani wa Sh milioni 20....ipo mifano mingine Rais ameitaja, anahitaji kuungwa mkono ili huduma za kijamii ziboreshwe,” alisema.

Alisema pamoja na mishahara mikubwa lakini baadhi ya watumishi wana posho na marupurupu makubwa, matumizi mabaya ya magari ya ofisi, nyumba na simu za kiofisi kwa shughuli binafsi na kwamba iwapo Rais Magufuli atasimamia suala hilo maisha ya Watanzania yatabadilika.

Source: Habari leo
 
HV hii nchi ni gani mbna ina makundi makundi kama c yetu vile kwahy mbunge kusema hvyo ishakuwa habari kwa kuwa ni wa mawazo mbadala...tusimame tujenge nch yetu makundi ya mitaloni tupa kule.
 
Sioni tatizo kumpongeza mapadlock....

kama amefanya vyema na asifiwe tu..wala sio dhambi
 
Sawa lakini mwambie kutanguliza maslahi ya Chama yatamualibia kwani wenye demokrasia Yao wakali Sana
 
Back
Top Bottom