Mbunge wa CCM alia njaa Jimboni kwake mbele ya Polepole

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay, amemuomba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kufikisha kilio cha wananchi kwa Serikali ili wapatiwe chakula cha njaa.

Massay amesema hayo leo baada ya Polepole kufanya ziara ya siku mbili wilayani Mbulu ya kukagua uhai wa chama, kusikiliza kero na kuzungumza na Halmashauri Kuu ya CCM, wilaya ya Mbulu.

Amesema hivi sasa wananchi wana wakati mgumu kutokana na bei ukame uliokea msimu uliopita hivyo Serikali iwapatie chakula cha bei nafuu.

Amesema wananchi wa eneo hilo ni hodari kwa kulima mazao mbalimbali ya chakula na biashara, ila kutokana na ukame uliotokea msimu uliopita hivi sasa wanakabiliwa na upungufu wa chakula.

"Kwa sababu chama ndiyo kinasimamia Serikali, kilio hiki cha wananchi tunakifikisha kwako ili tatizo lao limalizike, kwani wanataka chakula cha bei nafuu na siyo chakula cha bure", amesema Massay.

Chanzo: Mwananchi
 
Cha ajabu wakiwa bungeni wanakaa kimya kuhusu njaa.

Inamaana wanapima upepo kwa ile kauli kuwa Tanzania hakuna njaa
Tatizo la wabunge wa ccm wako pale bungeni kwa ajili ya kuitetea serikali,ikitokea wabunge wa upinzani wakatoa hoja yenye kutetea wananchi,wao wataipinga kwa nguvu zao zote na kutoa vijembe na kejeli huku wakishangiliana na kugonga meza
 
Jamani njaa ipo Kenya tena siyo yote baadhi ya sehemu. Huyo mbunge ni mvivu anapenda vya rahisi
 
Serikali haitatoa Chakula cha bure msemakweli ni mpenzi wa Mungu, fanyeni Kazi, hapa kazi tu by sizonje
 
Angefikiri kwanza wapi apeleke kilio cha wananchi wake na si kuibuka tu kama uyoga.
 
Kala maharage ya wapi huyo? Yaonekana hamjui sawa sawa "mwajiri wake"! Haiwezekani amlipe mshahara halafu amkosee adabu vile.Ajiandae!
 
Njaa lazima itangazwe na kutambuliwa na Dereva wa Lori na siyo mbunge. Hapo hakuna njaa.
 
Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay, amemuomba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kufikisha kilio cha wananchi kwa Serikali ili wapatiwe chakula cha njaa.

Massay amesema hayo leo baada ya Polepole kufanya ziara ya siku mbili wilayani Mbulu ya kukagua uhai wa chama, kusikiliza kero na kuzungumza na Halmashauri Kuu ya CCM, wilaya ya Mbulu.

Amesema hivi sasa wananchi wana wakati mgumu kutokana na bei ukame uliokea msimu uliopita hivyo Serikali iwapatie chakula cha bei nafuu.

Amesema wananchi wa eneo hilo ni hodari kwa kulima mazao mbalimbali ya chakula na biashara, ila kutokana na ukame uliotokea msimu uliopita hivi sasa wanakabiliwa na upungufu wa chakula.

"Kwa sababu chama ndiyo kinasimamia Serikali, kilio hiki cha wananchi tunakifikisha kwako ili tatizo lao limalizike, kwani wanataka chakula cha bei nafuu na siyo chakula cha bure", amesema Massay.

Chanzo: Mwananchi
Huyo mbunge kweli ni kanjanja yaani kilio cha wananchi ndio akipeleke kwa polepole?nimeamini wabunge wa ccm wengi ni chumia tumbo tu yeye anashindwa nini kuongea hayo bungeni hasa kipindi hiki cha budget?
 
Tatizo la wabunge wa ccm wako pale bungeni kwa ajili ya kuitetea serikali,ikitokea wabunge wa upinzani wakatoa hoja yenye kutetea wananchi,wao wataipinga kwa nguvu zao zote na kutoa vijembe na kejeli huku wakishangiliana na kugonga meza
Hawajitambui na hawafai
 
Siasa mpaka 2020
Sijaribiwi.

CHADEMA anzeni kukagua uhai wa chama na ninyi halafu ajitokeze kubwa jinga aanze kutoa povu tuone.

Tume huru idaiwe mapema Tanzania ccm itoke.
 
Back
Top Bottom