Nucky Thompson
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 1,817
- 4,059
Mbunge wa Sumbawanga mjini Aeshi Hilal ameitaka serikaliiruhusu viroba viuzwe hadi vimalizikie stock iliyobaki, kwa kuwa imewapa hasara kubwa wafanyabiashara ambao wengine wamekopa benki na kuwasababishia kufilisika hadi mwingine wa huko Dodoma kujiua.
Ameongezea pia askari wamekamata viroba vingi na wamefikia kuvinywa viroba hivyo vinapokuwa vimehifadhiwa
Mwanasheria mkuu wa serikali Masaju amesema kuwa suala hilo lipo mahakamani kwa hiyo mahakama itakavyoamua ndio itakavyokuwa, na amesema hatua ya kuvipiga marufuku ni nzuri kwani wananchi wengiwameipongeza serikali kwa kuwa vilikuwa vikiathiri afya na utendaji wa wengi