Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
MBUNGE JULIANA MASABURI AKIZUNGUMZA NA VIJANA KATIKA BARAZA LA UVCCM WILAYA YA ILALA, DAR ES SALAAM
"Tunaamini fursa mnazijua, elimu mmepewa na mmezipokea lakini jukumu letu sisi viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) ni haya mafunzo tuliyopata twende tukawape na wengine, tusikae nayo sis pekee yetu, tuwashirikishe na Vijana wengine" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa
"Wote tunatambua mambo makubwa yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Juzi hapa Wilaya ya Ilala imezinduliwa Treni ya Mwendokasi (SGR, Standard Gauge Railway), ni mambo mengi yamefanyika Mkoa wa Dar Es salaam hasa Wilaya ya Ilala" - Juliana Didas Masaburi
"Ili Chama Cha Mapinduzi kiweze kushika dola ni lazima kiwe na Wanachama. Mkoa wa Dar Es Salaam ni kama lango la nchi yetu, uchaguzi wa Serikali za Mitaa ndiyo moyo wa Chama na Serikali. Naomba Vijana tufanye kazi kwa pamoja tupate ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unaotarajiwa Kufanyika Mwezi Novemba, 2024" - Mhe. Juliana Didas Masaburi
"Niwaombe ndugu zangu Vijana wa Chama Cha Mapinduzi twende tukatoe elimu chini kwa Vijana wenzetu ili wajitokeze kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na pia tuongeze juhudi za kujiandikisha kwenye mfumo wa kielektroniki (TEHAMA)" - Mhe. Juliana Didas Masaburi