Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,675
Kama kuna mtu bado alikua na imani kidogo na watu wa CCM jana amejionea mwenyewe, wakati Rwanda na nchi nyingine wamejitahidi kutafuta watu wenye uwezo kwenda kupigania nchi yao CCM wamefanya ushabiki wa kitoto usio na msingi wowote kwa kupiga hapana dhidi ya wagombea ambao Watanzania wote na dunia imeshuhudia uwezo wao.
Pamoja na chuki zao tumejitahidi kupiga kura bila chuki kwa kuweka mbele maslahi ya nchi yetu tumechagua watu walioonesha uwezo hata kama wanatokea CCM.Sisi kama chama kwetu Masha na Wenje walikuwa ni watu bora kutuwakilisha.
Kwa mfano Rwanda, nchi imewapeleka mawaziri wawili na Attorney General (AG) wao EALA ili wakapambanie maslahi ya taifa lao.Sisi tunafanya figisu na kubaki na hoja za vyama.Mataifa haya wataendelea ku-dominate uchumi wetu na kutuburuza kwenye mambo ya msingi.
Sisi tutabaki na hoja ya kuomba Kiswahili iwe lugha rasmi,inakera sana.