Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,140
- 1,982
Wanajamvi:Mbunge Wa Mwibara Mh.Kangi Lugora Amepinga Wapiga Kura Wa Jimbo Lake Kudaiwa Michango Ya Ujenzi Wa Maabara Kwa Kuwa Jimboni Kwake Na Mkoa Wa Mara Kuna Njaa.Mkuu Wa Wilaya Ya Bunda Mh.Mirumbe Amekemea Kitendo Hicho Na Kusema Ni Cha Mtu Asiye Na Akili.Nani Kati Yao Hana Akili?Source ITV
Wadau,
Ikumbukwe kuwa wakuu wa wilaya wamepewa jukumu la kuhakikisha fedha za ujenzi wa maabara zinakusanywa kutoka kwa wananchi maskini bila kujali hali zao. MaDC hao wakaenda mbali zaidi na kutoa kalipio kuwa yeyote atakayekwamisha zoezi hilo ataonja sero na hatimae gerezani kama hatapata dhamana. Hii haijalishi ni Mbunge, Diwani, Mwenyekiti wa mtaa au Kijiji na pia mwananchi yeyote yule.
Leo katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku iliyorushwa na ITV kutoka Bunda imemuonesha Mh. Kangi Lugola mbunge wa Mwibala pamoja na Mh. Ezekiel Maige mbunge wa Msalala wakihamasisha wananchi kugoma kuchanga michango ya ujenzi wa maabara. Wabunge hao walienda mbali na kuwaambia wananchi kuwa haiwezekani kutumikia mabwana wawili (1. Njaa na 2. Ujenzi wa maabara). Ndipo swali likaulizwa nani anaweza kutumikia mabwana wawili?
Wakati huo huo ikarudiwa taarifa ya Mkuu wa wilaya ya Bunda aliyetoa kauli ya kumchukulia hatua mtu yeyote atakayegomesha wananchi kuchagia ujenzi wa maabara.
My take
Ni muda muafaka sasa kwa mkuu wa wilaya ya Bunda kutenda alichoongea (walk2talk) ili tuone ubavu wake wa kumuweka ndani (SERO) Mh. Lugola na Mh. Maige.
Fanya faster Mheshimiwa DC ili mgawane kitambaa cha bendera ya CCM.