Mbunge Ally Kessy ataka mbwa, mbuzi, kuku, ng'ombe, baiskeli zilipiwe kodi

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Mbungewa Nkasi Kaskazini Ally Kesi amezungumzia suala la kulipa kodi na kutaka mifugo kama kuku, mbwa, ngombe zilipiwe kodi, ametaka pia vyama vya siasa vikatwe kodi kwenye ruzuku vinayopewa kutoka serikalini

Mbunge huyo pia ameponda tabia ya rais kujiamulia kugawa mikoa na majimbo bila vigezo vinavyoeleweka na kuongeza gharama na ametaka serikali ipitie upya majimbo na mikoa ipunguzwe ili kupunnguza gharama.

Ametolea mfano wa mkoa wa Kilimanjaro ambao ni mdogo una majimbo 9 wakati mkoa wa Rukwa una majimbo 5.
 
Huyu mbunge wa CCM anamlalamikia nani sasa kama jimboni kwake hamna maji ni uzembe wake.
Wabunge wa CCM kipindi hiki cha kukatwa kodi kwenye mafao yao wana hasira sana wanataka mpaka baiskeli ilipiwe kodi.
 
Mimi sijaelewa hivi wabunge wanalipa kodi katka posho wapewazo!? maana taarifa inasema watalipa kodi kiinua mgongo na sio posho na mishahara yao ,kwa mujibu wa sheria walioipitisha iliwapa msamaha wa kutokulipa kodi .Naomba kueleweshwa.
 
Kuku walipiwe kodi?, mbwa walipiwe kodi?, duuuh kweli sasa ni hapa kodi tu kumbe sio hapa kazi tu
 
Hawa wamechanganyikiwa kwahiyo saizi wanataka hadi mbuzi ziwe zinalipa kodi.
Yani hapo kweli watakuwa wameishiwa pointi kwasababu ukipiga hesabu hela ambayo wanachukua kwenye dawa za mifugo ni nyingi sana na zinawatosha.
 
Mimi naunga mkono tena kodi iwe kubwa Tu, kwa kuwa matatizo tuliyokuwa nayo sasa yamechangiwa na wao kuwapigia kura watu wasiofaa
 
Hivi kweli tuna watetezi uko Bungeni? Mbona wanaongea viti vya ajabu kiasi iki? Nano atatetea wananchi wenye hali ya chini wakati Mbunge wake anapendekeza aendelee kunyonywa vizuri?
CCM tumewakosea wapi hadi muanze kutaka kuturudisha enzi za Ukoloni?
Mmeiba,mmefisadi kila kona sasa hivi mnataka ata kile kidogo tulichonachi mkichukue.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom