Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Wakuu huyu hawa wabunge kutwa wanafikiria kunyoosha njia zao wanasajisahau sana, kuna mwingine alitaka bima yao irefushwe kupita muda wa kawaida kisa anaogopa akiugua akiwa kwenye kampeni wakati hou kipindi chote alipata mshahara mnono na Pensheni la kucheba.
Leo Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba jina amependekeza wabunge wapewe 'plates number' maalumu zitakazowatambulisha barabarani kwenye misafara au kwenye shughuli zao za kila siku, ili wakiwa barabarani wapishwe na wafike haraka huko waendako, changamoto zetu wananchi mtazionea wapi kama mnataka kujitenga na sisi wananchi wa kawaida? Kinondoni Oktoba mjitafakari sana.
"Kuna wabunge ambao tunatoka kwenye mikoa ambayo hatuwezi tukapeperusha bendera, kwa mfano wabunge tunaotoka Dar es salaam na naamini hata tukiwepo Dodoma, hatupeperushi bendera na tukienda Zanzibar hatuwezi tukapeperusha bendera.
Sasa inatokea wakati kuna misafara ya kitaifa hata ya kimkoa ambapo tunatakiwa tufike maeneo fulani kwa uharaka ama saa nyingine tunakuwepo kwenye ile misafara lakini kwa kuwa magari yetu hayana utambulisho wowote ule, kwa mfano mimi najizungumzia sisi tunaotaka Dar es salaam magari yetu hayana utambulisho wa aina yoyote hatuwezi tukapeperusha bendera, tunajikuta katika orodha ya watu ambao wamo katika msafara, labda pengine gari yako inawekwa nyuma kiasi kwamba wanaofikia pale mbele ukiitwa mbunge njoo utoe salamu ndiyo kwanza unatafuta sehemu ya kupaki.
Sasa nilikuwa nafikiria kama kanuni ya kupeperusha bendera inaweza ikaendelea, Je bunge haliwezi likafikiria labda tunaweza tukawa na 'number plates' kwamba mtu unachagua gari lako moja ambalo ungelitumia kwenye shughuli zako za kikazi likawa na 'Number plates' inayoashiria kwamba gari hili ni gari la mbunge ili kuweza kusaidia mahali ambapo anatakiwa afike haraka ili barabarani ukikutana na traffic ukajieleza bwana mimi nawahi mahali fulani ama hata ukiwepo katika misafara ili usiweze ukaharibu 'protocal' za misafara ukawa unawahi na gari yako ikapewa heshima ya kuwepo pale ili uweze kutekeleza wajibu wako wa kibunge."
Tarimba ameyasema hayo katika mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine leo Juni 11, 2025 Bunge linatarajiwa kupitisha azimio la Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanuni za Bunge kuhusu marekebisho ya kanuni za Bunge.