singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Hivi karibuni kikao cha baraza kuu cha Chadema kilichofanyika jijini Mwanza kulisikika majigambo kutoka kwa Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Edward Lowassa.
Katika majigambo hayo wawili hao walieleza jinsi chama chao kilivyoongeza idadi na wabunge na kura za rais hivyo kuongeza kiwango cha fedha za ruzuku kutoka serikalini, huku wakidai kupunguza kiasi cha fedha za kila mwezi, walizokuwa wakipata CCM.
Ni kweli Chadema imeongeza wabunge na kupata kura nyingi za rais tofauti na chaguzi zilizopita, mambo ambayo yatakifanya chama hicho kuongeza pia kiasi cha fedha za ruzuku kutoka serikali.
Hata hivyo, pamoja na majigambo hayo viongozi wa juu wa chadema juu ya chama chao kuongeza fedha za ruzuku kutoka serikalini, je kuna azimio lolote la kikao hicho cha Baraza kuu kilichofanyika Mwanza kinachoeleza mkakati ya wowote wa chama hicho kumiliki adhri na kujenga majengo yake ya ofisi zake, walau katika ngazi ya mkioa ya wilaya ?
Je ongezeko hilo la fedha za ruzuku kutoka serikalini lina faida gani kwa mwanachama na wafuasi wake, kama fedha hizo za ruzuku haziwezi kununua ardhi ya chama kwa ajili kujenga ofisi ya kudumu zinazomilikiwa na chama ngazi ya mkoa na wilaya?
Ni mjumbe gani, kutoka mkoa gani ambaye alijifikirisha kuhoji suala hilo la chadema kuwa na ofisi za kudumu badala ya ofisi za kupanga katika majumba ya watu kama inavyofanyika sasa?
Kama hakuna mjumbe yeyote aliyejifikirisha kuhoji, Je viongozi wa juu wa Chadema akiwemo Mbowe na Lowassa wao hawaoni umuhimu wa kuwa na ofisi za chama chao ili kurahisisha mawasiliano ya wanachama na wafuasi wa chama chao?
Ongezeko la fedha za ruzuku kwa Chadema kutoka serikali lina faida gani kawa chama cha siasa kama hazitafanya kazi za chama kama vile kujenga ofisi zake, badala yake zikaishia kwenye mifuko ya viongozi wakuu wa chama waliopo makao makuu, mtaa wa Ufipa Kinondoni, Dar Es Salaam?
Nawasilisha.