Mbowe: Madaktari msiende Kenya, Rais anacheza na maisha yenu, Kenya sio salama kwa sasa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
SEHEMU YA II - CHADEMA tunasema hivi, Rais Magufuli acha mchezo wa kucheza na maisha ya madaktari wetu, katika mazingira ya kawaida, ingekuwa wanakwenda Kenya wakati kuna hali ya utulivu, kuna hali ya uhakika wa Usalama Kenya tungeruhusu vijana wetu wakafanye kazi kwa sababu hata Wakenya ni ndugu zetu, lakini katika mazingira ambayo kuna mgomo Kenya, kuna kutoelewana kati ya Serikali ya Kenya na madaktari wao, sisi ndio tuwe kimbelembele cha kuwatoa watoto wetu kwenda kutibu Kenya wakati Wakenya wenyewe hawawataki ni kuweka maisha ya Watanzania wenzetu , wataalam wetu katika risk, sisi Kama Chama Kikuu cha Upinzani tunapinga, na naomba Mkutano huu Mkuu wa Kanda ya Pwani utoe tamko la kupinga madaktari wetu kwenda nchini Kenya.

Magufuli na Serikali yake wawape ajira vijana wetu vituo vya afya havina madaktari, Sera yetu ya Taifa inasema vituo vyetu vya afya lazima vihudumiwe na madaktari lakini mpaka leo hakuna madaktari kwenye vituo vya afya kwa sababu Serikali imeshindwa kuajiri.

Kwa hiyo wapo vijana wengi kwa muda wa miaka miwili hawajaajiriwa lakini suluhu sio kuwakimbizia nchi za jirani ambazo zina migogoro na wataalam wao, suluhu ni Serikali yetu itafute fedha iwaajiri vijana hawa, mama zetu, wazee wetu, vijana wetu wanawahaitaji madaktari hawa wawatibu katika vituo vyetu vya afya katika zahanati zetu katika hospitali zetu, Kwa hiyo naomba Mkutano Mkuu Maalum wa Kanda Pwani, naomba mnikubalie Kama Mwenyekiti wa Chama kupitia Mkutano huu tutoe tamko hili rasmi la kupinga madaktari wetu kwenda nchini Kenya.

Nimecopy kwa @FreemanMboweTz
 
Nikichangia nitaitwa mpinzani kwa vile kayasema Mbowe, lakini kama mtanzania ninayewatakia heri wenzangu naomba niseme. Tangu Jana nimetafakari sana kusudio la kupeleka watanzania wenzetu Kenya kuchukua nafasi za madaktari waliogoma. Tufikiri kidogo kabla ya kufikia hitimisho hili. Watapokelewaje na wale walioko kwenye mgomo ambao serikali sasa inatafuta mbadala ili kuweka rehani ajira zao? Usalama wao utalindwa na nani muda wote? Je, hii si sawa na kupeleka madaktari wetu vitani tena vita ya wenyewe kwa wenyewe (serikali vs madaktari)? Madaktari wakenya watawatazama watz kwa jicho jeupe huku wakiamini wako upande wa serikali.? Je, msaidizi wa adui yako aweza kuwa rafiki yako? Tutafakari pamoja.
 
Ushauri umeshibaaaaa kabisaaaaa
466e0622dca4283a61b8d1e6699fc457.jpg
90c4e678b816c9edd967476e914afa9f.jpg
57e7cdf7f78530d37fde9c9857ade1c6.jpg

Kwa sasa kidogo nna amani maana jembe la sheria africa nzima tundu lissu kawashika pabaya!!!
 
Rais Mkapa alikataa kupeleka wanajeshi qetu kule Congo na kauli yake naikumbuka: sitaki kupokea majeneza. Haya ya Rais wetu 'kuwpeleka' madaktari amabao hawana ajira wala mkataba wowote na serikali ni kiini macho cha kuwapeleeka katika matatizo na kisha wakipata shida wanabaki wakiwa. Sijui hata kwa nini tunatumia kauli ya kuwa Tanzania inapeleka madaktari?
 
SEHEMU YA II - CHADEMA tunasema hivi, Rais Magufuli acha mchezo wa kucheza na maisha ya madaktari wetu, katika mazingira ya kawaida, ingekuwa wanakwenda Kenya wakati kuna hali ya utulivu, kuna hali ya uhakika wa Usalama Kenya tungeruhusu vijana wetu wakafanye kazi kwa sababu hata Wakenya ni ndugu zetu, lakini katika mazingira ambayo kuna mgomo Kenya, kuna kutoelewana kati ya Serikali ya Kenya na madaktari wao, sisi ndio tuwe kimbelembele cha kuwatoa watoto wetu kwenda kutibu Kenya wakati Wakenya wenyewe hawawataki ni kuweka maisha ya Watanzania wenzetu , wataalam wetu katika risk, sisi Kama Chama Kikuu cha Upinzani tunapinga, na naomba Mkutano huu Mkuu wa Kanda ya Pwani utoe tamko la kupinga madaktari wetu kwenda nchini Kenya.

Magufuli na Serikali yake wawape ajira vijana wetu vituo vya afya havina madaktari, Sera yetu ya Taifa inasema vituo vyetu vya afya lazima vihudumiwe na madaktari lakini mpaka leo hakuna madaktari kwenye vituo vya afya kwa sababu Serikali imeshindwa kuajiri.

Kwa hiyo wapo vijana wengi kwa muda wa miaka miwili hawajaajiriwa lakini suluhu sio kuwakimbizia nchi za jirani ambazo zina migogoro na wataalam wao, suluhu ni Serikali yetu itafute fedha iwaajiri vijana hawa, mama zetu, wazee wetu, vijana wetu wanawahaitaji madaktari hawa wawatibu katika vituo vyetu vya afya katika zahanati zetu katika hospitali zetu, Kwa hiyo naomba Mkutano Mkuu Maalum wa Kanda Pwani, naomba mnikubalie Kama Mwenyekiti wa Chama kupitia Mkutano huu tutoe tamko hili rasmi la kupinga madaktari wetu kwenda nchini Kenya.

Nimecopy kwa @FreemanMboweTz

Ninamuheshimu na kumkubali sana Mheshimiwa Freeman Alkaeli Mbowe japo Mimi ni Mwana CCM niliyetukuka ila nadhani kuna mahala katika maelezo yake kidogo ametokota na inaonyesha pia hakumsikiliza vizuri Mheshimiwa Rais JPM na hata Waziri husika juu ya hao Madaktari 500 wanaokwenda nchini Kenya.

Ni kwamba Madaktari ambao watapewa Vipaumbele kwenda nchini Kenya ni wale wa Sekta binafsi ambapo ndipo naamini kuna Kundi kubwa la Madaktari ambao bado hawajapata Ajira ila Tangazo hili au Fursa hii haiwahusu Madaktari wote wa Serikalini na walio katika Mikataba maalum.

Ni vizuri siku nyingine Mheshimiwa Mbowe akatuliza kwanza Kichwa chake pale anapotaka kutolea ufafanuzi jambo fulani ambalo kimsingi linahitaji utulivu na uchambuzi wa kutukuka kabisa katika kulikabili.
 
Mimi nakubaliana na msimamo wa Mbowe na Chadema. Hata hivyo tutafakari ukata unaolikabili taifa kama matokeo ya siasa mbovu na uongozi hovyo. Kam serikali haiwezi kuajiri sasa, kicha ya mahitaji makubwa ya madakidari katika vituo vyetu vya afya, ni busara kwa serikali kutangaza kuwa kuna ajira kenya na kila mwenye kuhitaji ajira aombe at one's own risk. Ni makosa kwa serikali kuahidi kupeleka madakidari kwa kuamini ahadi za makipo nazuri na ulinzi. Hebu anayetaka kazi aombe mwenyewe, madakitari wa kenya wenye hasira kali sababu ya mgogoro uliopo/ uliokuwapo, wakiamua kumdhuru dakitari toka TZ serikali yetu isijeingia lawamani. Wasi wasi wasi wangu ni uwezekano wa kuongeza chuki dhidi ya madakitari wetu na serikali yetu.

Serikali itafute pesa iajiri vijana wetu. Wananchi wanyonge wanawahitaji sana madakitari wetu.
 
Nadhani mh Mbowe ana point kwakuwa si kweli kwamba Kenya ina upungufu wa madaktari ila ni ubabe tu wa serikali yao kutosikiliza mahitaji ya madaktari wake
Achana na wale madaktari waliogoma, kenya inamadaktari wengine 1400 ambao hawana ajira

Hawana upungufu wa madaktari ila wamegoma sababu ya maslahi
 
Ningeshauri serikali ya kenya ikiwachukua basi iwe uraia kabisa waonekane nao ni wakenya
 
Back
Top Bottom