Mbowe, Lowassa na Sumaye kuteka nchi - Ziara ya Mkoa kwa Mkoa

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,228
MKAKATI wa kuteka nchi unapangwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), anaandika Happiness Lidwino. Ni kwa kufanya ziara nchi nzima kwa lengo la kukukumbusha wananchi kwamba, nchi inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri. Kumekuwepo na malalamiko kwamba, Rais John Magufuli anaendesha nchi kinyume na taratibu pia Katiba ya Nchi na kwamba, ziara hiyo imepangwa ili kuzindua wananchi wajibu wa kudai viongozi waongoze kwa mujibu wa Katiba ya Nchi.

Ziara hiyo imepangwa kuanza kutekelezwa tarehe 7 Juni mwaka huu. Ziara hiyo itaanzia mkoani Shinyanga, Wilaya ya Kahama. Baada ya hapo kutakuwa na timu mbili zitakazozunguka katika mikoa yote nchini ikiwemo ya Chato, Bukoba, Geita, Sengerema, Muleba, Meatu, Bunda, Bariadi na kumalizika Mwanza ambapo timu hizo mbili zitakutana.

Akizungumza na waandishi leo Jijini Dar es Salaam Mkurungenzi wa Oganezesheni na Mafunzo wa CHADEMA, Kigaila Benson amesema, timu hizo mbili pia zitafika katika nyanda zote nchini zikiongozwa na viongozi wote wa chama akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe,Katibu Mkuu Dr Vicent Mashinji wajumbe wa Kamati kuu na mawaziri wakuu wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya chama na kisha ziara hiyo kumalizikia Dar es Salaam.

Benson amesema, kwa kuwa Chadema ni chama kikubwa cha upinzani kina haki ya kufanya ziara hiyo ya kuwafumbua macho na kuwaelimisha wananchi juu ya uongozi anaodai wa kidikteta unaofanywa na Rais Magufuli.
“Tangu kuingia madarakani Rais Magufuli kumekuwa na ukiukwaji wa sheria na katiba, serikali imekuwa ya mtu mmoja na maamuzi ya mtu mmoja kana kwamba, hakuna wizara husika kitu ambacho kinawakandamiza wananchi na kushindwa kupata haki zao,” amesema.

“Hatuta choka kupiga kelele anapoenda kinyume na kupuuza Katiba ya nchi na tunataka wananchi wa mtambue na wajue namna ya kudai haki zao.
Tangu kuingia kwake madarakani hakuna maendeleo zaidi ya kulipiza visasi kwa watu ambao hawakumuunga mkono wakati wa kampeni.
“Rais Magufuli amevunja na kuvuruga vitu vingi vilivyopo kwenye Katiba ikiwepo sikukuu, kupanga matumizi ya fedha wakati wizara husika zipo, uvurugaji wa bunge na mengine mengi yasiyomuhusu,” amesema.

Aidha Benson amesema kuwa, wananchi nchini wajiandae kupewa elimu ya utambuzi na kuanza kuchukua hatua juu ya utendaji wa mtu waliyempa dhamana ya kuwaongoza. Pia amesema tayari wameshatoa taarifa katika vyombo vya usalama na hivyo wananchi wasiwe na shaka.
 
MKAKATI wa kuteka nchi unapangwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), anaandika Happiness Lidwino. Ni kwa kufanya ziara nchi nzima kwa lengo la kukukumbusha wananchi kwamba, nchi inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri. Kumekuwepo na malalamiko kwamba, Rais John Magufuli anaendesha nchi kinyume na taratibu pia Katiba ya Nchi na kwamba, ziara hiyo imepangwa ili kuzindua wananchi wajibu wa kudai viongozi waongoze kwa mujibu wa Katiba ya Nchi.

Ziara hiyo imepangwa kuanza kutekelezwa tarehe 7 Juni mwaka huu. Ziara hiyo itaanzia mkoani Shinyanga, Wilaya ya Kahama.
Baada ya hapo kutakuwa na timu mbili zitakazozunguka katika mikoa yote nchini ikiwemo ya Chato, Bukoba, Geita, Sengerema, Muleba, Meatu, Bunda, Bariadi na kumalizika Mwanza ambapo timu hizo mbili zitakutana.

Akizungumza na waandishi leo Jijini Dar es Salaam Mkurungenzi wa Oganezesheni na Mafunzo wa CHADEMA, Kigaila Benson amesema, timu hizo mbili pia zitafika katika nyanda zote nchini zikiongozwa na viongozi wote wa chama akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe,Katibu Mkuu Dr Vicent Mashinji wajumbe wa Kamati kuu na mawaziri wakuu wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya chama na kisha ziara hiyo kumalizikia Dar es Salaam.

Benson amesema, kwa kuwa CHADEMA ni chama kikubwa cha upinzani kina haki ya kufanya ziara hiyo ya kuwafumbua macho na kuwaelimisha wananchi juu ya uongozi anaodai wa kidikteta unaofanywa na Rais Magufuli.
“Tangu kuingia madarakani Rais Magufuli kumekuwa na ukiukwaji wa sheria na katiba, serikali imekuwa ya mtu mmoja na maamuzi ya mtu mmoja kana kwamba, hakuna wizara husika kitu ambacho kinawakandamiza wananchi na kushindwa kupata haki zao,” amesema.

“Hatuta choka kupiga kelele anapoenda kinyume na kupuuza Katiba ya nchi na tunataka wananchi wa mtambue na wajue namna ya kudai haki zao.
Tangu kuingia kwake madarakani hakuna maendeleo zaidi ya kulipiza visasi kwa watu ambao hawakumuunga mkono wakati wa kampeni.
“Rais Magufuli amevunja na kuvuruga vitu vingi vilivyopo kwenye Katiba ikiwepo sikukuu, kupanga matumizi ya fedha wakati wizara husika zipo, uvurugaji wa bunge na mengine mengi yasiyomuhusu,” amesema.

Aidha Benson amesema kuwa, wananchi nchini wajiandae kupewa elimu ya utambuzi na kuanza kuchukua hatua juu ya utendaji wa mtu waliyempa dhamana ya kuwaongoza. Pia amesema tayari wameshatoa taarifa katika vyombo vya usalama na hivyo wananchi wasiwe na shaka.
 
Mkuu Molemo

Nashukuru sana kwa taarifa hii mujarabu. Kusema la ukweli hakuna mtawala aliyewahi kuendesha inchi kiimla huku akivunja katiba na sheria mbalimbali. Ktk hili #BabaJesca ataumbuka mapema sana.

Safi sana CHADEMA. Tuko pamoja sana
 
Duh! Kweli tumepoteza mechi kama taifa staaa.
Kwahiyo hiyo Agenda ya Jamaa hafuati katiba ndio tunaingia nayo mkoa na kifua cha tongwa! Hakuna agenda nyingine maana Ile ya Ufisadi ilitupwa mtaroni?
Usiweweseke CCM imefeli mapema sana
 
BabaJesca tumekuaachaaa mnoooo ufanye siasa peke yako, sasa ni muda uanze kupata upinzani mkali.

Maana ulikua peke yako, sasa hivi ni jino kwa jino
 
Asante sana ITV television ya Taifa namwona hapa comrade Benson Kigaila akiweka mipango dhahiri dahiri mbele ya umma.

Huwezi kuendesha nchi kwa hisia na mbwembwe as if unaongoza familia yako. Shame to you #BabaJesca na serikali ya mafisiemu
 
Hii ni babkubwa acha sasa tuone Magufuli akijibu hoja za makamanda kutokea uraiani maana bungeni wamebana. Kila laheri makamanda tunawasubiri huku uraiani na vile pesa inashindana na sukari kwa kuhadimika hakika ni muda muhafaka sasa.
 
Back
Top Bottom