makonda piaMagufuli bila polisi ni raisi mf
Mtaenda the HAGUE mkaliwe ndogo na kina Chales tayrol,,,na huyo mnyarwanda wenukwani ukiambiwa umeshika dola maana yake nini? unashika dola bila polisi au jeshi au? kushika dola huko chadema tafsiri yenu huwa nini?
we jamaa mweupe sana kichwani. Kwani Gadafi si na yeye alikuwa umeshika dola kama unavyosema.kwani ukiambiwa umeshika dola maana yake nini? unashika dola bila polisi au jeshi au? kushika dola huko chadema tafsiri yenu huwa nini?
Uchaguzi kinondoni magu ajipime kutokurusha bunge uongozi wake kwa jumla yupo sahihi au afikirie upya ili watu wamueleweChaguzi hizi ndogo zinazoendelea hapa nchini zinathibitisha kwamba hali ya Chama Cha Mapinduzi ni mbaya sana licha ya Mwenyekiti wake wa Taifa kujitahidi kuwaaminisha watanzania kuwa yeye ni Rais bora na Rais pendwa.
Nguvu inayotumiwa na vyombo vya dola kuibeba CCM ni kubwa Sana, kwa bahati mbaya sana CCM wanadhani kuwa watanzania ni wajinga na malimbukeni lakini kimsingi watu wanajua na wanatambua kila linaloendelea. Mambo haya Yana mwisho wake
Tz hakuna uchaguzi nimaigizo tu haiwezekani kila kitu wapange ccm alafu mtegemee haq nisawa na kusubiri embe chini ya mnazi labda iletwe na mafurikoMKUU POLIS WENG WANATOKA CHAMANI
Timiza ahadi yako mwenyekiti.
Mwenyekiti Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa katika uchaguzi huu mdogo wa marudio katika majimbo mawili ya Kinondoni na Siha jeshi la polisi liandae magereza ya kutosha kwani watawafunga wote na kudai hawawezi kukubali kura kuibiwa.
Ameyasema hayo kwenye kampeni za CHADEMA Magomeni jijini Dar es salaam ambapo amedai Chama Cha Mapinduzi (CCM) bila polisi ni wepesi na hawawezi chochote sababu chama hicho kimeshapoteza mvuto kwa wananchi.
“Yaani nyinyi polisi muachie CCM dakika tano tu wacheze ngoma siku ya tarehe 17 hawa jamaa ni weupe, na polisi ndugu zangu safari hii mtuandalie magereza mtatufunga wote haki ya Mungu, safari hii haibiwi mtu kura hiyo nawaambia mtatuua. Kama tumeweza kupona risasi 38 sasa tupo tayari kwa lolote, Wabunge wetu wanafungwa, wanafukuzwa Bungeni, madiwani wanalazimishwa kuhama chama, kila siku viongozi wa upinzani ni polisi na mahakamani,”amesema Mbowe
Hata hivyo, Mbowe amesema kuwa endapo watafanyiwa mambo ambayo walifanyiwa kwenye uchaguzi wa Kata 43 basi mambo hayawezi kuwa mazuri
Chanzo: Dar24