Barabara ya Old Moshi inayoanzia barabara kuu iendayo Dar es Salaam kupitia Kiboriloni Primari, kijiji cha Kikarara, kijiji cha Tsuduni hadi kijiji cha Kidia (km 19.8) katika Kata ya Old Moshi Mashariki, pia ni ahadi nyingine ya Rais aliyoitoa wakati wa kampeni za 2010 eneo la Tsuduni na imeingizwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa 2011-2016, alisema Chami.
Inaelekea ahadi ya barabara hii hata haifahamiki kabisa, kwa sababu hata katika taarifa mbalimbali kwa viongozi wa kitaifa wanaotembelea Kilimanjaro haisikiki. Kumbe nimeona niukumbushe uongozi wa Tanroads mkoa na wa Wizara ya Ujenzi juu ya barabara hii, japo natambua uwapo wa mawasiliano kati ya Mama Anna Mkapa (mzaliwa wa Kijiji cha Kikarara) na Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli juu ya ujenzi wa barabara hii, alieleza Chami.