Mbowe alitunishia misuli jeshi la Polisi...!!

Mbowe alitunishia misuli jeshi la Polisi...!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana alihojiwa tena na Jeshi la Polisi, lakini akaendelea na msimamo wake kwa kugoma kuwasilisha ushahidi wake kuhusu mlipuko wa bomu uliotokea mkoani Arusha Juni 14, mwaka huu.
mboye+px.jpg


Mbowe alifika Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam kuitikia wito wa jeshi hilo kumtaka awasilishe ushahidi

wake aliosema kuwa anao, lakini aligoma akisema atautoa pale tume ya kijaji itakapoundwa na Rais Jakaya

Kikwete kama alivyoomba.

Kiongozi huyo wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alitaka kuundwa kwa tume huru ili kuchunguza mlipuko huo

uliotokea alipokuwa akihitimisha hotuba yake katika mkutano wa mwisho wa kampeni za udiwani kwenye

Viwanja vya Soweto, Arusha.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika alisema jana kuwa Mbowe alikwenda polisi baada

ya kuandikiwa barua ya kumtaka afike kuwasilisha ushahidi. Alifika lakini aligoma kutoa ushahidi huo.

"Alikwenda tu kuitikia wito wa polisi uliomtaka awasilishe ushahidi, lakini amegoma kufanya hivyo na amewaeleza polisi kuwa hatafanya hivyo hadi Rais atakapounda tume ya kijaji kama alivyomwandikia barua," alisema na kuongeza: "Anachosubiri sasa ni majibu ya Rais kuhusu barua yake."

Mnyika alisema baada ya maelezo hayo, Mbowe alitakiwa kuyaweka kimaandishi kupitia kwa wakili wake

Peter Kibatala na kuyawasilisha polisi ifikapo kesho.

Akizungumzia suala hilo, Wakili Kibatala alisema: "Mbowe ameachiwa baada ya majadiliano ya

kisheria kati yangu na Kamanda Advocate Nyombi. Tumekubaliana kujibu kwa maandishi wito wa

polisi walioutoa kwake wakimtaka awasilishe ushahidi wa kuhusika kwa polisi katika mlipuko wa

bomu Arusha na kisha kuyafanyia kazi hayo kisha kutuarifu
."

Msemaji wa Polisi SSP, Advera Senso alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema anafuatilia kujua kama kweli

Mbowe alihojiwa na kama kutakuwa na habari ya kuwajulisha wananchi ataitoa baadaye.

Wiki iliyopita jeshi hilo lilimhoji Mbowe kwa madai kuwa kauli zake alizozitoa baada ya mkutano wa Kamati

Kuu ya chama hicho ni za uchochezi.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai alihojiwa kutokana na madai aliyosema kwamba polisi ndiyo

waliohusika na ulipuaji wa bomu Arusha, pia polisi kusaidia CCM kwenye uchaguzi na kumtuhumu Rais

Jakaya Kikwete kuhusika na mauaji ya Arusha kutokana na kukaa kwake kimya.



 
mbona tume zingine huwa zinaundwa fasta tu soon after tukio? Kwa hili la arusha ni nini kinampa kigugumizi mkuu wa kaya? hapo hata mi naona kuna ihusika wake tene wa moja kwa moja, au ndo wanaandaa kwanza majibu halafu ndo waunde tume? Kwa hili ccm na polisi wenu hamtoki, hii ngumi imewageukia ninyi tena ya kichwa.......mmeua watu wasio na hatia,damu zao kaburini zitawalilia daima,hivi kwanini msikubali tu kuwa cdm saiv inapendwa? Kila kitu kina mwanzao na mwisho kubalini huu ndo mwisho wenu mkae bench mjipange 2020 mje na sera nzuri tutawachagua tu lakini mambo ya kuua watu yanawapa laana tu,tena mby zaidi mnaanza kusingizia kwa wengine
 
Bichwa vya habari vingine vinaweza kumponza mtu, Eti mbowe alitunishia msuli jeshi la polisi? Vichekesho kweli!!! Wakimminya kidogo mnaanza kulia na kuchonga.
 
Namuunga mkono Mbowe kwa hili kwa asilimia 100, ila tu awe na ushahidi usio na mashaka, or else itamletea shida katika kuaminika siku za usoni.
Natamani kumuona mtani wangu, Mwigulu Nchemba akiingia jela--Singida hatuwezi kukubali kuwa watanzania wa kwanza kutoa "Hitler". God forbid!
 
Natoa wito kwa Mbowe , asiende tena polisi , ni usumbufu tu hawana jipya , kaa mbali nao wasijekukuwekea mionzi bure !
 
Jesh la police bwana yan wanakuwa kama watoto.
Hivi mh Mbowe asingelisema anaushahid wa tukio lile la Arusha ndo ingelikuwa imetoka?
Je, wenyewe wamechunguza nn kama wanategemea ushahid wa mbowe?
 
Mbowe amewatega pabaya. Unadhani Raisi atathubutu kuunda hiyo tume?
Akiunda ikathibitika ni kweli serikali ya CCM imehusika unadhani itakuwa ripoti nzuri kwao?
 
Back
Top Bottom