Mbowe agonga mwamba kortini, hata TLS watagonga mwamba!

Mka
Ni juavyo mimi CCM hajawahi kuwa na rafiki wa kudumu,
CC: Lowassa, Rostam, Nape, Membe, Malima, Masha, Mramba, Yona, Sumaye, Mgeja, Diallo n.K
Ccm haijawahi kuwa rafiki wa kudumu kwa wananchi wote wa kipato cha chini.
 
Mleta uzi hata kama serikali imeshinda kwako unaona ni sawa upuuzi aliokuwa anafanya Bashite uendelee??

Hizi sheria kandamizi kabisa unazitetea vipi ndugu?
Mkuu;
Kumlaumu 'Bashite' ni kutomtendea haki kwa sababu yeye aliapa kusimamia sheria.

Ifahamike kuwa kama sheria ni mbovu, kazi ya kuzibadilisha niya wabunge wakiwamo kina Tundu Lissu. 'Bashite' sio Mbunge.

Sheria kandamizi zinabadilishwa bungeni.
 
Tumeshachoshwa na mambo yako ya kuokoteza okoteza ili kuutetea uhalifu wa serikali. Tunaona unavyofurahia udhaifu wa katiba ambayo ilitungwa na hata kuwekwa viraka viraka ambavyo vyote vilimuacha mkuu akiwa na madaraka ya kupitiliza. Wewe endelea kutetea mfumo kwa sababu kwa sasa unakushibisha. Daima sisi tutaendelea kuupigania mfumo ule ambao utaweka haki sawa na wajibu kwa wote.
 

Kwa hiyo kutimiza majengo kwa Serikali ni kunyanyasa RAIA na si kutenda haki na kutotumia madaraka vibaya??

Kama ni hivyo basi ndani ya Serikali kuna matatizo makubwa sana.
 

Kwa hiyo kutimiza malengo kwa Serikali ni kunyanyasa RAIA na si kutenda haki na kutotumia madaraka vibaya??

Kama ni hivyo basi ndani ya Serikali kuna watendaji wenye matatizo makubwa sana.
 
Taratibu we mtu, acha mbwembwe! Mbowe kabwagwa kivipi? Mahakama imesema haina mamlaka (Jurisdiction) ya kusikiliza shauri husika, na sio kwamba shauri halina mantiki kisheria! Hivyo hapa ni swala la kuhamishia kwenye mahakama yenye mamlaka hayo na huko ndo itajulikana mbivu na mbichi! Sasa hivi ni mapema mno kwako kushangilia!!!
 
Hii kesi ilifunguliwa na mbwembwe nyingi
Ni kama ulivyoanzisha thread kwa mbwembwe nyingi utafikiri katika dunia na Tanzania nzima ni Mbowe tu ndiye wa kwanza kushindwa kesi na hakuna mtu mwingine ambaye alishawahi kupeleka pingamizi Mahakamani na kushindwa.
 

Huyo hajielewi,maana upande ni kama anatamani Sheria kandamizi zifutwe upande anaona kama Mbowe atafanikiwa.Hivyo issue nani kapeleka kesi kwake ndiyo tatizo,angepeleka Tulia au Mwakyembe ni sawa.
 
Haki sawa uipate hapa duniani? You must be joking!

Hata mbinguni hakuna haki sawa. Kumbuka hata mbinguni kuna wengine wamekaa karibu na kiti cha enzi wakati wengine wako mbali.

Mathayo 4:17
Na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni mwanangu, mpendwa wangu ninayependezwa naye.
 
Mkuu;
Mimi ni hata vitabu vya sheria na langi zake sizifahamu.

Nilitumia komoni sensi tu katika kuchanganua mazingira ya kisheria.
Sasa ameshindwa au mahakama imeigwaya kesi?
 
Mkuu;
Kwani kazi ya polisi ni nini? Hujui kuwa hizo pesa zinazotumika ndivyo zimepangwa kwa kazi hiyo.

Kushinda kwa Lissu au kutoshinda sio kazi ya polisi bali ni kazi ya mwanasheria wa serikali.
Kumbe wewe bure kabisa! Hivi mwanasheria wa serikali ndio huwa anaagiza kakamate Fulani?
 
Hata mbinguni hakuna haki sawa. Kumbuka hata mbinguni kuna wengine wamekaa karibu na kiti cha enzi wakati wengine wako mbali.
Hapa sasa unatumia akili ya kibinadamu kufasiri habari za Mwenyezi Mungu. Hekima hii huna.
 
Uhai wa chadema unategemea mafanikio ya sarakasi za Lisu. Lisu akishindwa sera ya chadema itakua imefeli akishinda sera ya chadema itakuwa imefaulu. Ni aibu sana chama kongwe kama Chadema kubakia kutegemea mafanikio ya sarakasi za mtu mmoja.
 
Kama lingekuwa ni tatizo dogo nadhani viongozi wote wakuu wa CHADEMA wasingehamia mahakamani.

Inawezekana wewe unadhani ni tatizo dogo lakini viongozi wako wakuu wana mtazamo tofauti.


Eti kabisa naye Ulimwengu ni wakili serious wa kumwakilisha mtu.....ngachoka miyeπŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›
 
Eeeeh

Na mbwembwe zote kumbe hata wanasheria wao hawajui sheria..kazi wanayo wataiangalia Ikulu kwa mbali milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…