Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Mbona hawa watetema, wakubwa wanatetema,
Wapo wanahema hema, midomo imeachama,
Na meno yanawauma, mwili ukiwatetema,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Wamejipanga mamia, makumi ya mia na mia,
Kwa zamu wahutubia, ahadi wakimwagia,
Huku wakitukania, mioyo ikiwakimbia,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Mbuyu ukitikisika, ni mwanzo wa kuanguka,
Mizizi itachomoka, chini "puu" kusikika,
Si punje itaokoka, majani yatapukutika,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Nimeshika togwa miye, nakunywa naangalia,
Nasubiri nisikie, walotetema wanalia,
Ujumbe uwafikie, imebadilika Tanzania,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Walidhani hakuchwi, sasa kumbe kumepambazuka.Elimu ya uraia kwetu,imegeuka sumu kwao,
Hotuba za nyerere tamu,wao zimegeuka nyongo,
Hata wazee vidole viwili juu, Kijani hazivaliki hata kiteto,
Hahahahahaha! nimejaribu!
Mbona hawa watetema, wakubwa wanatetema,
Wapo wanahema hema, midomo imeachama,
Na meno yanawauma, mwili ukiwatetema,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Wamejipanga mamia, makumi ya mia na mia,
Kwa zamu wahutubia, ahadi wakimwagia,
Huku wakitukania, mioyo ikiwakimbia,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Mbuyu ukitikisika, ni mwanzo wa kuanguka,
Mizizi itachomoka, chini "puu" kusikika,
Si punje itaokoka, majani yatapukutika,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Nimeshika togwa miye, nakunywa naangalia,
Nasubiri nisikie, walotetema wanalia,
Ujumbe uwafikie, imebadilika Tanzania,
Waone waweweseka, na pia wanatetema,
Na upepo haujavuma? Ukivuma ni anguko!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
tena wanawaya waya, nguo zinao uzani,
bora wangesoma aya, singewindwa ka kunguni,
wajapoimbiwa kwaya, pepo lipo kiunoni,
na upepo haujavuma, ukivuma ni anguko.
ukivuma ni anguko, kutowesha vichokoo,
kama wa kisulisuli, ole ni kwa zao koo,
ghiliba zimewakatili, sasa wanaona soo,
chama kongwe mapinduzi, kimejipindua pindu.
Kumbe nawe "mayu" mkali kweli kweli"
Nadhani hapo kwenye "mayu" unabahatisha!!!!!!
Kweli inawezekana nabahatisha, je nimepatia?