masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,173
- 13,776
Tatizo la mauaji ya watendaji, wanasiasa, polisi na wengine mkoani Pwani yanaanza kuchukua sura mpya. Sura mbaya ya ugaidi.
Tunakumbuka yale ya Amboni ,Tanga. Serikali iliyachukulia matukio ya Tanga kwa uzito uliostahili, na sasa yamekuwa historia.
Haya matukio ya mkoa wa Pwani, karibu kabisa na makao makuu ya kila Idara ya usalama nchini, yanatia wasiwasi.
Watu waingie kazini, wasingojee kupewa ripoti tu ya matukio.
Kuliachia jeshi la polisi peke yake kwa matukio haya ni kulipuuzia tishio hili la kile kinachoonekana kuwa ni kajipu kanakojitokeza ka ugaidi.
Katumbuliwe kabla hakajaleta madhara makubwa katika jamii.