John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 110
- 210
Mbinguni kuna makao mangapi
Wakati Bwana Yesu alipokaribia kuondoka duniani, alisema:
Yohana 14:1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo.
Kwa mara ya kwanza Yesu aliwafunulia wanafunzi wake, kuhusu mambo yaliyo kwa Baba yake tuliyoandaliwa sisi. Na hapo anasema huko kuna “makao mengi”. Hasemi kuna
“kao” kama kwamba ni moja, bali “makao”, tena mengi. Hatujui idadi, labda ni mia, au elfu, au milioni. Yesu kusema mengi, amini ni mengi kweli kweli. Yesu Hasemi uwongo.
Aina ya makao mbinguni
Kwa kuchambua yaliyoandikwa kwenye biblia, tunaweza kuona kuwa kuna makao ya aina tatu. Moja, alituletea tayari, lakini mengine mawili yatakuja baadaye.
Kao la kwanza
Hili lilikuwa ni yeye kutukaribisha ndani yake.
Hilo lilitimia muda mfupi sana, baada ya kuondoka duniani. Tunaona baada ya siku 10, siku ile ya pentekoste, alirudi tena juu yetu, kama Roho Mtakatifu. Akaingia ndani yetu. Kwa mara ya kwanza sisi ndio tulipokea mahusiano binafsi ya moja kwa moja na Mungu, tukaingia nyumbani mwake.
Hii imeandikwa katika Matendo 2: 1 "Hata ilipotimia siku ya Pentekoste, walikuwako wote mahali pamoja. 2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka".
Mtu aliye na Roho Mtakatifu, huishi tofauti na mtu ambaye hana Roho Mtakatifu. Kwa sababu ulimwengu wake ni mwingine kabisa na ule wa kwao. Kao lako ni kuu zaidi ya kao lao la kidunia. Raha na pumziko analolipata, walimwengu hawawezi kulipata. Hekima na upeo ulionao wewe, wale hawana. Hakika kao hili ni zuri sana. Unapojazwa Roho vema, ndiyo unaona uzuri wa kao hilo maishani mwako.
Kao la pili
Ni kao la roho zetu.
Kumbuka roho hizi zipo ndani ya miili hii ya mavumbi. Lakini Yesu aligundua udhaifu wa miili hii. Hivyo, alikwenda kutuandalia miili ya utukufu itokayo juu, ambayo hiyo tutavishwa, siku ile ya unyakuo itapofika, miili ambayo haijatengenezwa kwa malighafi za duniani, bali zile za mbinguni. Miili isiyozeeka, isiyougua, isiyo sikia njaa, wala isiyokufa. Ni kao zuri ambalo hakuna hata mmoja wetu anapaswa alikose.
Kitabu cha 2Wakorintho 5 kinasema: 1 "Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni. 2 Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; 3 ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi. 4 Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima".
Kao la Tatu
Ni mazingira mapya ya watakatifu. Ndiyo ile mbingu mpya na nchi mpya.
Na ule mji wa mbinguni, Yerusalemu mpya, ishukayo kutoka juu kwa Baba. Uzuri ulioko huko hauna kifani. Ni mji unawaka na kumeta-meta utukufu wa Mungu.
Hii imeandikwa katika Ufunuo 21: 15 "Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake. 16 Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa. 17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika. 18 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi. 19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; 20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto.
21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.
22 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.
23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.
24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake. 25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku. 26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.
27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo".
Hayo ni makao matatu tu, mbinguni. Vipi kuhusu hayo mengine ambayo hatujafunuliwa? Ukiyajua hayo, hutauchukulia wokovu kirahisi-rahisi, utafanya bidii uingie ndani ya Kristo.
Tumekwishaambiwa waziwazi, kuwa kuna makao mbinguni. Tumeambiwa pia kuwa makao hayo ni mengi, na yamekwenda kuandaliwa.
Tunachotakiwa kufanya ni kumfuata Kristo ili atupe uzima wa milele, ili kutuwezesha kuishi kwenye makao yake mbinguni.