mbeya medical research programme

xiande

Member
Oct 3, 2012
90
12
wanajamii hivi kwa wale ambao waliomba mmrp kuna ambao wameshaitwa kwa interview??
 
dah watu humu ndani huwa tunaingizana machaka na ukiwasikiliza wengine unaweza ukazimia bureeee....mdau juu acha uwongo kama hujui khaa kimya mimi jana walinipigia simu wakaniambia leo niende kufanya interview na kulikuwa na watu kibao tu !
 
Kaka mimi sibaatishi mambo clas met wangu aliyekuwa anafanya field pale ameaajiriwa hata wikimbil hazijaisha kama unabisha we siumeitwa intvw uliza mtu mmoja anaitwa John Joseph kama lab scientist utapewa jibu
 
Hii ni post yangu ya kwanza,nimekuwa interested na hii topic,to the extent....,ebu tuambie huyu jamaa alikuwa classmate wako wapi na kamaliza chuo gani?
 
dah juzi pia wengine walifanya interview pia...!mwenye update za waliofanya last week km washaitwa??
 
Nimeshawahi fanya kazi Mbeya Medical Research Programme, ambayo sasa inaitwa Mbeya Medical Research Center; baada ya NIMR kuichukua kwa sehemu kubwa. Ni kituo cha kwanza nchimi Tanzania kuanza kufanya tafiti kubwa na nzuri za chanjo ya kuzuia ugonjwa wa UKIMWI. Utafiti wao wa kwanza wa hii chanjo walianza mwaka 2005.
Kilikuwa kituo chenye uwezo mkubwa kifedha kwa kuwa ilikuwa ni sehemu ya Idara ya tropical medicine katika chuo kikuu cha Munich, Germany.
Serikali kupitia NIMR taratibu imekuwa inakichukua kituo hiki, nao wajerumani taratibu wanajitoa. Hii imesababisha kucheleweshwa kwa mishahara na upungufu mwingine wa pesa katika idara mbalimbali. Lakini mishahara yao ni mizuri kuliko serikalini hata kuwazidi sana kituo cha utafiti Ifakara.
Kwa sasa ni kituo ambacho hakitabiriki kama kitaweza kujiendesha au la, kwa kuwa wanaotafuta pesa ndio wanakabidhi kituo taratibu.
Kuhusu utoaji kazi, huwa wako wazi sana, ingawa hupendelea zaidi kuwapa kazi wale waliofanya nao field au wale waiojitolea, kwa kuwa wanakuwa wanajua utendaji wao.
Sijui kama serikali ina ubavu wa kutafuta pesa kuendesha taasisi hii na pia sijui kama watanzania wana maono ya kutengeneza tafiti kubwa zenye mashiko, la sivyo kituo hakieleweki kitaishia wapi.
Ubaya wa Wajerumani ilikuwa kufanya publications peke yao, kutoa mishahara kwa utofauti mkubwa bila kujali sifa, kubana nafasi za kujiendeleza kimasomo, kuwanyima watanzania taarifa za ndani kuhusiana na tafiti kwa ujumla na pia kuwaweka wajerumani wenzao kuwa viongozi wa vitengo ijapo hawana sifa huku watanzania wenye sifa wakiwepo.
 
Back
Top Bottom