Mbeya manispaa oneni hili

Mbeya manispaa oneni hili

Heron

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2013
Posts
1,946
Reaction score
1,804
Habari wakuu.

Naomba niende moja kwa moja kwenye Mada yangu.
Nimekuwa na safari za Nyanda za juu kusini. Yaani Mbeya
Na nimekuwa nikitembelea soko Maarufu la Mwanjelwa.
Ajabu ni kuwa Hili soko ni zuri sana la kisasa ila naweza kusema halina wafanya biashara.

Na ni sehemu ndogo sana ya jengo iliyopangishwa. Almost asilimia zaid ya 70 lipo wazi..

Nionanyo Mimi hii ni kama hasara kwa Manispaa ikizingatiwa kuwa huenda gharama za ujenzi zikawa ni Mkopo kutoka katika Mabenk yetu. Au hata kama ni za serkali
Sasa kwa hali hii vipi wataweza kupata faida kutokana na uwekezaji walioufanya?.

USHAURI
Ukizunguka upande wa nyuma wa soko kuna eneo kubwa sana ambalo lipo reserved kama parking.

Je kwakuwa ukiangalia Mbeya ni kama Haina stand nzuri ya Bus za Mikoani hasa kwa town ukiacha ile ya Nane nane.
Kwanini wasiangalie uwezekano wa kulibadilishia matumizi jengo hilo na kuwa Stand ya Mabasi?

Hasa kutokana na nafasi kubwa iliyopo ndani ya uzio wa jengo la soko , wangifanyaiwe kama stand ya Muda ya Bus za Mikoani tu.
Bila ya shaka Vile vyumba vyoote (Frame) zitapata wapangaji ( Booking office) ,
Tena zitagombaniwa kuanzia juu mpaka chini.

Huku mbele wayaache Mabenk kama yalivyo.
Zile gates ndogo zinakuwa za kupitia abiria ambapo watatengeza utaratibu kama wa Ubungo wa tickets za tsh.200/300 kwa kila abiria asiye na ticket au msindikizaji.
Gari ndogo ziwe na bei yake +buses.

Sina shaka baada ya Miezi 6 huenda Wakawa tayar wamerejesha pesa yao + kama walichukua loan wakawa tayar wame clear.

Halafu uzuri mbele ya jengo kuna stand ya Daladala .
Kwahiyo itakua nje daladala ndani Buses.

Fanyieni kazi kama itawafaa maana naona kama pale ni Hasara tu .
Nawasilisha
 
Ulichokisema hakiwezekani campus ya pale ndani ni ndogo kwa mabus kukaa pale......
 
Pale biashara inasua sua pamj na kodi kuwa juu..kwa kifuph watu wanapaogopa wanajua gharama ni kubwa
 
mbeya mji wangu wa historia. mbaliz ndipo nilipoanzia maisha baada ya kurud bongo. daa nimekumbuka minadan. kamsamba, santiria ilembo mkwajuni. wazee wa utengule mpoo!?. umenikumbusha mbali sana. niliupenda sana huo mji. ni miaka 15 sasa cjafika nikijaliwa nitarud mbeya.
 
Santiriya na Ilembo duh! Kitambo sana naipenda sana ile miji
mbeya mji wangu wa historia. mbaliz ndipo nilipoanzia maisha baada ya kurud bongo. daa nimekumbuka minadan. kamsamba, santiria ilembo mkwajuni. wazee wa utengule mpoo!?. umenikumbusha mbali sana. niliupenda sana huo mji. ni miaka 15 sasa cjafika nikijaliwa nitarud mbeya.
 
Back
Top Bottom