Timu za msimu tu hizo na kila mwaka huwa zinakuwepo tangu ligi ikitambulika kama Ligi Daraja la Kwanza.
Zilikuwepo:
Reli Morogoro, Mecco, Tukuyu Stars, Coastal Union(enzi za kina Bakari Tutu), Pamba (TP Lindanda)
Baadaye zikatokea Ushirika Moshi(enzi za kina Mwakitope), Milambo (enzi za kina Wastara Baribari), Majimaji, Mtibwa Sugar na hawa Prisons
Kizazi hiki zimeibuka Azam FC, Kagera Sugar na sasa nawaona Mbeya City wanakuja juu katika huu mzunguko wa kwanza.
Sina uhakika kama wataweza kuwa juu hivi ikifika duru la pili na miaka ijayo, lakini nikiangalia historia naona kama haipo upande wao hivyo nahisi kama ni upepo tu uvumao na utapita.