Mbelwa Mohamed Mustafa

mwanamama

Member
Feb 6, 2008
61
0
Wandugu nina taarifa yenye uthibitisho kuwa jamaa aliyemuua bro Raymond Tungu Kapalata ameshikwa jana jumamosi saa saba mchana huko Iringa Tanzania, baada ya kukimbia kutoka Mwanza ambako alishiriki kwenye ugomvi. Vyanzo vyetu vya habari vinatuambia kuwa jamaa yuko mbaroni na ubalozi wa Marekani Dar umekwishataarifiwa,ili afanyiwe utaratibu wa kurudishwa Marekani kuja kujibu mashtaka ya mauaji.
Ikumbukwe kuwa ni miaka mitatu sasa toka ndugu yetu Ray alipotutoka, madhali muuaji ameshakamatwa sheria itachukua mkondo wake.
Na wale ndugu zetu ambao mko Detroit MI msisite kutoa taarifa yoyote ambayo itaelekeza kukamatwa kwa waliowaua ndugu zetu Nkya na Mazula. Kwa sababu ndugu hawa wameuliwa na watu, kwa hiyo ni lazima sheria ichukue mkondo wake.
Habari ya kukamatwa kwa muuaji wa Ray imeandikwa pia kwenye YoungAfrican.com
 
Asante sana kwa taarifa na tunashukuru Mungu kakamatwa huyo muuaji. Ray bado alikuwa kijana mdogo aliyekuwa anajitafutia maisha yake.
 
Mbali na huyo muuaji kukamatwa lakini inabidi tujiulize na kujifunza kwanini watz wauane kwenye nchi za watu??? chanzo ni nini? kwanini watu wasiishi kama ndugu???? Nafikiri kuna tatizo.
 
Wandugu nina taarifa yenye uthibitisho kuwa jamaa aliyemuua bro Raymond Tungu Kapalata ameshikwa jana jumamosi saa saba mchana huko Iringa Tanzania, baada ya kukimbia kutoka Mwanza ambako alishiriki kwenye ugomvi. Vyanzo vyetu vya habari vinatuambia kuwa jamaa yuko mbaroni na ubalozi wa Marekani Dar umekwishataarifiwa,ili afanyiwe utaratibu wa kurudishwa Marekani kuja kujibu mashtaka ya mauaji.
Ikumbukwe kuwa ni miaka mitatu sasa toka ndugu yetu Ray alipotutoka, madhali muuaji ameshakamatwa sheria itachukua mkondo wake.
Na wale ndugu zetu ambao mko Detroit MI msisite kutoa taarifa yoyote ambayo itaelekeza kukamatwa kwa waliowaua ndugu zetu Nkya na Mazula. Kwa sababu ndugu hawa wameuliwa na watu, kwa hiyo ni lazima sheria ichukue mkondo wake.
Habari ya kukamatwa kwa muuaji wa Ray imeandikwa pia kwenye YoungAfrican.com

Wewe ulisema Mbelwa Mohamed Mustafa amekamatwa vipi mbona kimya au Interejensia yako haikuwa na uhakika?
 
Leo nimeona instagram page ya dada yake na muuaji wa Ray Kapalata RIP bi Cynthia Masasi akimuwish Happy birthday kaka yake kwa kutomtaja jina na kumpa jina mtu mrefu Yahya Toure. Hivi mlioko ughaibuni states hii kesi iliishaje ?
 
Back
Top Bottom