GE2025 Mbatia ataka mazungumzo ya Kitaifa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

GE2025 Mbatia ataka mazungumzo ya Kitaifa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ametoa wito kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa nchini, wakiwemo wa CHADEMA, CCM, na ACT-Wazalendo, kuonesha ukomavu wa kisiasa kwa kuweka kando tofauti zao na kukutana kwa mazungumzo ya pamoja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam siku ya Ijumaa, Mbatia amesema kuwa kuna haja ya kujenga maridhiano mapema badala ya kusubiri hali ya sintofahamu itokee au kutafuta lawama baada ya madhara kutokea.

Ametahadharisha kuwa kupotea kwa maisha ya mtu mmoja katika muktadha wa kisiasa ni hasara isiyoweza kurekebishwa, na hivyo ni muhimu kila upande kuwa na utulivu wa fikra na kutumia nafasi iliyopo ya mazungumzo.

Ameeleza kuwa bado kuna nafasi ya kufanya maridhiano ya kweli, ikiwa ni pamoja na kujadili uwezekano wa kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi iwapo itahitajika, ili kuhakikisha mazingira ya uchaguzi yanakuwa huru, ya haki, na yenye amani.

Kauli hiyo imekuja wakati ambapo hali ya kisiasa nchini inaendelea kushika kasi kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025, huku baadhi ya wanasiasa na makundi ya kiraia wakitoa maoni tofauti kuhusu mazingira ya uchaguzi na mustakabali wa demokrasia ya Tanzania.

 
Back
Top Bottom